Wednesday, July 31, 2024

MHE. SIMBACHAWENE AITAKA OFISI YAKE KUTOA USHIRIKIANO WA KIUTENDAJI KWA NAIBU WAZIRI SANGU ILI KUBORESHA UTUMISHI WA UMMA NCHINI

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 31 Julai, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa watumishi  pamoja na wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa ofisi yake kutoa ushirikiano wa kiutendaji kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu aliyeteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutumikia ofisi hiyo.

Mhe. Simbachawene ametoa wito huo leo jijini Dodoma, wakati wa hafla fupi ya kumpokea kiongozi huyo.

Mhe. Simbachawene amesema, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imepata kiongozi mwingine kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kiutendaji, hivyo ametoa rai kwa menejimenti ya ofisi hiyo kumpa ushirikiano wa kutosha ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu ili kufikia maono ya Rais wa Awamu ya Sita ya kuuboresha Utumishi wa Umma nchini.

“Tumepata kiongozi mwingine kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kiutendaji, niwatake mtoe ushirikiano kwa Naibu Waziri Sangu ili kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kutoa mchango katika Utumishi wa Umma kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” amesema Mhe. Simbachawene.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watumishi wote na kuongeza kuwa, atahakikisha anasimamia haki katika kufanya kazi.

Mhe. Sangu ameongeza kuwa, ataendeleza pale alipoishia mtangulizi wake katika kuujenga utumishi wa umma wenye uadilifu na unaowajibika kwa wananchi katika kutoa huduma bora ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuujenga utumishi wa umma unaowajibika kwa wananchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa pili kulia) akimkaribisha Naibu Waziri wa ofisi yake, Mhe. Deus Sangu (wa kwanza kulia) mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akipokea maua ya ukaribisho mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi ya Rais-UTUMISHI iliyopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa ofisi hiyo.


Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakisubiri kumpokea Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) kabla ya kuwasili katika ofisi hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa pili kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa ofisi yake Mhe. Deus Sangu (wa kwanza kulia) pamopja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi na Naibu Katibu Mkuu Bw. Xavier Daudi mara baada ya baada ya Naibu Waziri Sangu kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji mara baada ya Naibu Waziri huyo kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na sehemu ya watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wengine ni viongozi wa ofisi hiyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza jambo na mmoja wa watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa ofisi hiyo Mhe. George Simbachawene.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (wa tatu kushoto) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (wa pili kushoto) kabla ya kuwasili Naibu Waziri wa ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu aliyeteuliwa na kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa ofisi hiyo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli.












Monday, July 29, 2024

MHE. SIMBACHAWENE AKUTANA NA WENZA WA VIONGOZI WA KITAIFA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo kwa nyakati tofauti amewatembelea na kufanya mazungumzo mama Anna Mkapa na Janeth Magufuli nyumbani kwao Osterbay Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yake na wenza wa viongozi hao, Mhe. Simbachawene ameahidi kuwaelekeza watendaji katika ofisi yake, kushughulikia changamoto zinazojitokeza na kuwafanya wenza wa viongozi hao kuendelee kuishi kwa amani na usalama.

Aidha, Mama Mkapa amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kupata nafasi ya kumtembelea, kumjulia hali na kusikiliza changamoto alizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.

Vilevile Mama Janeth Magufuli amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake na kuwatunza wakati wote bila kuchoka na amemuombea kwa Mungu aendelee kuiongoza vyema Tanzania.







 

 

MHE. SIMBACHAWENE ATETA NA RAIS MWINYI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi nyumbani kwake Osterbay Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Simbachawene amemueleza Mhe. Dkt. Mwinyi kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza kumfikishia salaam kwa familia ya Hayati Ali Hassan Mwinyi na kuahidi kuendelea kuwa pamoja na familia hiyo kwa kuwa ni wajibu wa Ofisi yake kutunza wenza wa Viongozi wa Kitaifa na yeye yuko tayari kuendelea kutekeleza wajibu huo.

Mhe. Simbacahwene aliongeza kuwa anafanya ziara ya kuwajulia hali Wenza wa Viongozi hao ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Aidha, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameshukuru kwa ujio huo na kupongeza utaratibu uliopo wa kuwatembelea wanafamilia na kuwapa faraja.

 







Tuesday, July 23, 2024

TAASISI ZA UMMA KUFANYA UHAKIKI WA TAKWIMU ZA WATUMISHI WA UMMA WENYE VVU, UKIMWI NA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZA

 Na. Veronica Mwafisi-Manyara

Tarehe 23 Julai, 2024

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Cyprus Kapinga amezitaka Wizara na Taasisi za Umma kufanya uhakiki wa takwimu za watumishi wa umma wenye VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) ili kulinda afya za watumishi hao.

Bw. Kapinga ametoa wito huo leo wakati akifungua kikao kazi cha Robo ya Nne ya Mwaka 2023/2024 kilichoshirikisha Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa Mkoa wa Manyara wanaosimamia magonjwa hayo.

“Tunatakiwa kuwa na takwimu sahihi ya watumishi hao ili kurahisisha zoezi la kupanga bajeti ya kuwahudumia na kuimarisha afya ya akili na kudhibiti msongo wa mawazo. Watumishi hao ni sehemu ya nguvu kazi ya Taifa inayohudumia wananchi” alisisitiza Bw. Kapinga.

Aidha, Bw. Kapinga ametoa rai kwa Maafisa Masuuli wote katika taasisi za umma kuunda na kuimarisha Kamati za VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) zilizopo kwa kutoa nafasi kwa wanakamati hao kupata mafunzo na elimu itakayowafanya wawe na uwezo wa kushawishi watumishi kupima afya na hivyo kuwa na takwimu sahihi kwa  mipango bora na endelevu.

Awali akitoa neno la utangulizi, Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji aliwataka washiriki wa kikao kazi hicho kusikiliza na kufuatilila kwa makini mada zote zitakazowasilishwa ili wapate uwezo na ujuzi Madhubuti wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kupitia Idara ya Uendelezaji Sera ipo mkoani Manyara kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mapambano dhidi ya VVU, Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza (MSY) ili kuwalinda watumishi wa umma na kuhakikisha taifa linaondokana na vifo vitokanavyo na magonjwa hayo ifikapo mwaka 2030.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus Kapinga akizungumza na Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara wanaosimamia magonjwa hayo wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024.


Baadhi ya Wakurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) na Waratibu wa magonjwa hayo wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus Kapinga (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kinachofanyika mkoani Manyara.


Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus Kapinga kufungua kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 cha Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) kinachofanyika mkoani Manyara.

Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akitoa utambulisho wa Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara wanaosimamia magonjwa hayo kwenye kikao kazi kilichofanyika mkoani Manyara.


Afisa Maendeleo ya Jamii, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Neema Range akiwasilisha mada kuhusu Ujumuishwaji wa Sehemu za Anuai za Jamii wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kilichoshirikisha Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara.


Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi na Mratibu wa Kitaifa wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Juliana Ntukey akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Waraka wa kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza mahali pa kazi katika Utumishi wa Umma (2014) wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024.


Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY), Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara, Bi. Marietha Kyomo akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Manyara kuhusu hali ya utekelezaji wa Afua za VVU, Ukimwi na MSY wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kilichofanyika katika mkoa huo.


Mratibu wa Kinga na Mwitikio wa Kitaifa dhidi ya VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Dkt. Haffidh Ameir akitoa taarifa kuhusu hali halisi ya VVU na Ukimwi Nchini wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kilichoshirikisha Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara.


Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili, Dkt. Sadiki Mandari akiwasilisha mada kuhusu kuimarisha afya ya akili kwa Kamati ya Kifaifa, Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza (MSY) pamoja na Wajumbe, Wenyeviti, Makatibu wa mkoa wa Manyara wanaosimamia magonjwa hayo wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kinachofanyika mkoani Manyara.


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cyprus Kapinga akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Waratibu wa Wizara wa Kudhibiti VVU, Ukimwi na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) wakati wa kikao kazi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 kinachofanyika mkoani Manyara.



 

Thursday, July 18, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE APIGA MARUFUKU WATUMISHI WA UMMA KUSUMBULIWA KUFUATILIA TAARIFA ZA UHAMISHO

 Na Lusungu Helela - Kibakwe

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amepiga marufuku Watumishi wa  Umma  kusumbuliwa kufuatilia taarifa zao za kiutumishi wanapohamia kwenye kituo kipya cha kazi badala yake wafanye kazi zao kwani hilo sio jukumu lao bali ni wajibu wa Waajiri.

 

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na watumishi na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mlimo katika Kata ya Lufu, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma ambapo amesema suala la taarifa za Mtumishi ni jukumu la Mwajiri.

 

Amesema kitendo cha taarifa za watumishi kutohamishwa kumesababisha Watumishi hao kushindwa kupimwa kwenye mfumo wa e-tendaji kazi kwa vile kunakuwa hakuna taarifa za watumishi hao katika kituo kipya cha kazi na hivyo mwisho wake watumishi kusumbuliwa kufuatilia taarifa za kule walikotoka.  

 

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu- UTUMISHI kushirikiana na Mamlaka zingine zilikokasimiwa madaraka hayo ya kuhamisha Watumishi kuhakikisha Mtumishi pindi anapohama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine asisumbuliwe kuhusu taarifa hizo.

 

Hivyo Mhe. Simbachawene ametoa muda wa kuhamisha taarifa za watumishi waliohama kuwa ifikapo Agosti 15 mwaka huu taarifa za watumishi wote ziwe zimehamishwa na baada ya hapo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa wote watakaoshindwa kutekeleza jukumu hilo.

 

Amesema suala la kuhamisha taarifa za Mtumishi kutoka alikokuwa na kwenda kituo kipya cha kazi ni jukumu la Mkurugenzi au anayeongoza Taasisi wakishirikiana na Maafisa utumishi na kuongeza kuwa wanatakiwa kuhakikisha taarifa hizo zinahamishwa ndani ya mwezi mmoja ili watumishi waliohamishwa waendelee kufanya kazi zao kwa ufasaha.

 

"Utapimaje utendaji kazi wa mtumishi au kumpatia ruhusa mtumishi aliyepata dharula ilhali taarifa zake zipo sehemu nyingine, hii sio sawa, huko ni kuwatesa watumishi "amehoji Mhe. Simbachawene.

 

Amesema malalamiko ya kutohamishwa kwa taarifa za watumishi yamekuwa mengi kutoka kwa watumishi huku akiwataka watumishi wanapohama kutekeleza majukumu yao na hakuna atakayesumbuliwa.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza leo na watumishi na wananchi wa Kijiji cha Mlimo, Kata ya Lufu iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi.

Sehemu ya watumishi na wananchi wa Kijiji cha Mlimo, Tarafa ya Kibakwe iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, wakati wa ziara yake ya kikazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mlimo mara baada ya kuwasili, ikiwa ni ziara yake ya kikazi

Baadhi ya Madiwani wa Viti maalum wakiimba mbele ya   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya kumkaribishwa kwa ajili ya kuzungumza na  watumishi na wafanyakazi  katika eneo hilo

Diwani wa Kata ya Lufu Mhe. Gilbert Msigala akizungumza na wananchi wa  Kijiji cha Mlimo Kata ya Lufu iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya  Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Richard Maponda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mlimo, Kata ya Lufu iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.




Wednesday, July 17, 2024

JUKUMU LETU SOTE KUZINGATIA SHERIA KATIKA KUTOA NA KUPOKEA HUDUMA – Mhe.Simbachawene

 Na Mwandishi wetu - Kibakwe

 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, Mhe. George Simbachawene amewataka viongozi na wananchi kuzingatia Sheria za nchi katika kutoa na kupokea huduma.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Maswala na Kitongoji cha Ng'onje vilivyopo Katika Kata ya Pwaga, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa katika Jimbo hilo.

Mhe. Simbachawene amesema ili kuendeleza amani na kuepusha machafuko basi sheria za nchi ni lazima zizingatiwe na kila mtu awe kiongozi au mwananchi wa kawaida.

Amesema Tanzania imejengwa kwa misingi ya haki na usawa na ndio maana rasilimali za nchi zinagawanywa kwa usawa katika maeneo yote ya nchi ili kuchagiza utawala bora na ndio maana imeendelea kuwa kisiwa cha amani.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu ameendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuzingatia utoaji wa haki na usawa kwa wananchi wote bila kujali mahali walipo.

Ameongeza kuwa katika Jimbo la Kibakwe analoliongoza miaka ya nyuma vijiji vingi havikuwa na huduma nyingi za kijamii ikiwemo shule na zahanati lakini kwa sasa huduma hizo zote zipo maeneo mengi na wananachi wanaendelea kuhudumiwa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuhakikisha zinatoa kipaumbele cha huduma wanazozitoa kwa Taasisi za kijamii zilizopo katika Kata ya Pwaga.
 
Amesema huduma muhimu kama vile umeme na barabara ni muhimu zikafikishwa haraka katika maeneo ya shule, makanisa, misikiti pamoja na ofisi za vijiji.

Mhe.Simbachawene amesema Serikali imekuja na mpango mkakati wa ujazilizi ambapo vitongoji na maeneo yote ya pembezoni mwa miji itaanza kufikishiwa umeme.


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Pwaga, Mhe. Wilfred Mgonela ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Simbachawene kwa ushirikiano ambao ameendelea kumpa katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa katika Kata anayoiongoza huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana naye ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Kata kwa ujumla.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene   akizungumza leo na wananchi wa Kijiji cha Maswala, Kata ya Pwaga iliyopo katika Jimbo la Kibakwe,  Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa  ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi  katika Jimbo hilo.


 Sehemu ya wananchi wa Kitongoji cha Ng'onje kilichopo katika Kijiji cha Pwaga, Tarafa ya Kibakwe iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Maswala mara baada ya kuwasili, ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo hilo.

Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wa Tarafa y ya Kibakwe iliyopo katika  Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakitumbuiza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wananchi hao ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Diwani wa Kata ya Kibakwe Mhe.Wilfred Mgonela  akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Ng'onje cha Kijiji cha Pwaga Kata ya Kibakwe iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya  Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Richard Maponda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Maswala, Kata ya Kibakwe iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.


Thursday, July 11, 2024

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA JESHI LA POLISI KUHUSU MFUMO WA E-UTENDAJI KAZI



Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, SACP. Ibrahim Mahumi (Wa kwanza kulia) akizungumza na Timu ya Utekelezaji wa Mchakato wa Matumizi ya Mfumo wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Watendaji wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.

Kamishna wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Jeshi la Polisi DCP. Gabriel Semiono (Wa Pili Kushoto) akifafanua jambo baada ya kuwasilishwa kwa taarifa fupi ya namna ya upimaji wa utendaji kazi wa watendaji wa Jeshi la Polisi kwa sasa ili waweze kutumia Mfumo wa Tathmini ya Utendaji Kazi (e-Utendaji). Kikao kazi kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.


Mkurugenzi wa Huduma za TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango akifafanua jambo kwa Timu ya Utekelezaji wa Mchakato wa Matumizi ya Mfumo wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Watendaji wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, SACP. Ibrahim Mahumi (Wa kwanza kulia) akifuatilia wasilisho la namna Mfumo wa e-Utendaji kazi unavyofanya kazi wakati akiongoza kikao kazi cha mafunzo na majadiliano ya namna ya kutumia mfumo huo. Wa Pili Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Jeshi la Polisi DCP. Gabriel Semiono aliyeongoza Timu ya Utekelezaji wa Mchakato wa Matumizi ya Mfumo wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Watendaji wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Julai, 2024.