Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
George Simbachawene amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi
cha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imefanikiwa kuweka utaratibu wa mgao wa ajira unaotekelezwa kwa mujibu wa Waraka
wa Serikali wa tarehe 10 Mei, 2013 ambapo Tanzania Bara ni asilimia 79 na Tanzania
Zanzibar ni asilimia 21.
Ameyasema hayo leo Aprili 15, 2024 jijini Dodoma, wakati akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano kwa upande wa
Ofisi yake.
Amesema katika kipindi hicho cha miaka 60 ya Muungano, Ofisi ya
Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imekuwa ikifanya kazi kwa
ukaribu na Tume ya Utumishi wa Umma Zanzibar inayoratibu masuala ya ajira
katika watumishi wa umma ili kurahisisha zoezi la utangazaji wa nafasi za kazi
na upatikanaji wa watumishi.
Kutokana na ukuaji wa teknolojia, Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma imesanifu na kujenga mfumo wa kidijitali wa ajira Serikalini ambao
ni rafiki kwa watafuta fursa wote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa utengenezaji wa programu
ya rununu (Ajira Portal Mobile App) inayopatikana kwenye PlayStore na ApStore
za simu janja inalenga kuimarisha Muungano kwa kuwarahisishia waombaji wa fursa
za ajira kupata taarifa za uwepo wa fursa hizo kiganjani mwao mahali popote.
Katika hatua nyingine Mhe.
Simbachawene amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imedhamiria
kuondoa changamoto zinazowakabili waombaji wa fursa za ajira Tanzania Bara na
Zanzibar.
Aidha,
matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kipindi hiki cha miaka 60 ya Muungano imesaidia
waombaji kuepuka gharama za usafiri, malazi na changamoto za ajali, wakati Serikali
imepunguza muda wa usaili na gharama za uendeshaji wa zoezi hilo.
Mhe.
Simbachawene amewataka watafuta fursa za ajira wote kutoka pande mbili za
Muungano kufahamu akaunti zao, nywila na kuwa mahiri katika matumizi ya kompyuta
ili kuepukana na usumbufu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Miaka 60
ya Muungano wa Tanzania kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala bora leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya Waandishi wa Habari
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza kuhusu mafanikio ya Miaka
60 ya Muungano wa Tanzania kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa akitoa neon la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu
mafanikio ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania kwenye eneo la Utumishi wa Umma na
Utawala bora leo Jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa na baadhi ya
Wakurugenzi baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Miaka 60
ya Muungano wa Tanzania kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala bora, wa
kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Mary Mwakapenda
Baadhi ya Watumishi kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) wakimsiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu
mafanikio ya Miaka 60 ya Muungano kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala Bora.