Friday, June 30, 2023
Wednesday, June 28, 2023
WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA AJIRA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. George
Simbachawene akizungumza na watumishi ya
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) jijini
Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao
kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Sehemu ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watendaji hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Katibu wa
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Aliyesimama)
akielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George
Simbachawene (Meza
kuu katikati) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya
Sekretarieti ya Ajira kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Katikati) na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kulia) wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo mara baada ya kukabidhiwa maua ya ukaribisho wakati
alipowasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo jijini
Dodoma kwa
lengo la kufanya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji
kwa watumishi wa taasisi hiyo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea
maua ya ukaribisho mara baada ya kuwasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufanya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji.
Naibu
Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi
ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya
kuwasili katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo jijini Dodoma.
Naibu Katibu, Idara ya Ajira,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Lucas Mrumapili akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kufanya kikao kazi na watumishi wa Sekretarieti hiyo ya
Ajira kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja
na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na
watumishi hao kilichofanyika jijini Dodoma
kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Tuesday, June 27, 2023
Friday, June 23, 2023
WAZIRI MHE. SIMBACHAWENE AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUZINGATIA MIKATABA YA HUDUMA KWA MTEJA KATIKA KUTOA HUDUMA BORA
Na. Lusungu Helela-Dodoma
Tarehe 23 Juni, 2023
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene amewataka Watumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wananchi
huku akizitaka Taasisi zote za Umma kuhuisha Mikataba ya Huduma kwa Mteja kwani
ni nyenzo na kiungo muhimu katika kuboresha utendaji kazi kati ya Serikali na
Wananchi inaowahudumia.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 23, 2023 wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mhe. Simbachawene amewataka Watumishi hao kutambua kuwa wanapotoa huduma bora kwa wananchi wanamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza suala hilo mara kwa mara.
Kufuatia
hatua hiyo, amezitaka Taasisi za Umma kuzingatia Mikataba ya Huduma kwa Mteja katika
utoaji wa huduma kwa wananchi ili haki na wajibu wa pande zote mbili utendeke kwa
watoa huduma na wapokea huduma ambao ndio wateja.
Ameongeza
kuwa Ofisi yake ina wajibu wa kusimamia mifumo na viwango vya utendaji kazi
Serikalini kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa
wananchi na moja ya mifumo na viwango
vya Utendaji Kazi huo ni Mkataba wa Huduma kwa Mteja.
Awali,
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema
uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ni moja ya hatua muhimu ya kuboresha
huduma bora kwa wananchi ambapo amesema jumla ya Mikataba ya Huduma kwa Mteja
34 ya Taasisi za Umma imeweza kuzinduliwa.
"Uzinduzi wa mikataba hii ya Huduma kwa mteja inakwenda kuwezesha watumishi wa umma kuwa na utamaduni wa utendaji kazi unaojali matokeo na tija kwa wakati" amesema Mkomi
Aidha,
Katibu Mkuu Mkomi ametumia fursa hiyo kuzipongeza Taasisi za Umma ambazo
zimeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye maeneo yao kama ilivyoelekezwa na
Ofisi yake.
Naye,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Daudi Kandoro akitoa
neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa mikataba hiyo kwa niaba ya Wakuu wa Taasisi, amesema watatekeleza maagizo yote yaliyotolewa huku
akiahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilichoandikwa katika mikataba hiyo
ili wananchi waweze kujua wajibu na haki zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akizungumza na watumishi mbalimbali wa
Serikali pamoja na wananchi walioshiriki kwenye Uzinduzi wa
Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha
Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika
Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Bw.Juma Mkomi akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mikataba ya
Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho Wiki
ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere
Square Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Bw.Xavier Daudi akizungumza wakati wa
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika
Kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi cheti cha kuwa Mkataba wa Huduma
kwa Mteja uliokidhi viwango wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
wakati wa Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za
Umma katika Kilele cha Maadhimisho wiki ya Utumishi wa Umma ambayo
kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi
wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma
katika Kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo
kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Mhe.Rosemary Senyamule pamoja na viongozi wengine akiiaga kwaya ya Chuo
cha Utumishi wa Umma mara baada ya Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma
kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele cha Maadhimisho wiki ya
Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square
Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene wakati wa
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika
Kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akifurahia jambo na Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Juma Mkomi wakati wa
Uzinduzi wa Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma
katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa
yamefanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akiwa na baadhi ya Watumishi wakifurahi
mara baada ya kuzindua Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma katika Kilele
cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yamefanyika
katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji
wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akizungumza wakati wa utoaji vyeti na Tuzo
mbalimbali kwa Taasisi za Umma wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma ambayo Kitaifa yamnefanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Wednesday, June 21, 2023
Tuesday, June 20, 2023
Monday, June 19, 2023
Sunday, June 18, 2023
Saturday, June 17, 2023
SERIKALI YATOA RAI KWA WATUMISHI WA UMMA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI
Na. Lusungu Helela-Dodoma
Tarehe 17 Juni, 2023
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa rai kwa Taasisi Simamizi na Vyama vya Kitaaluma kuhimiza na kuwasimamia watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Watalaamu Waandamizi wa Taasisi Simamizi na Vyama vya Kitaaluma kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Bi. Shuli amesema kumekuwa na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi katika sekta ya afya, manunuzi, ujenzi pamoja na elimu ambayo yanahusu uvunjifu wa maadili, hivyo anaamini mafunzo hayo waliyoyapata kwa muda wa siku mbili yatasaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Kufuatia hatua hiyo, Bi. Shuli amezitaka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kujenga imani kwa wananchi na kuonesha thamani ya fedha zinazowekezwa na serikali katika miradi mbalimbali kwa kuwasimamia ipasavyo wataalamu wao katika utendaji kazi wao wa kila siku
‘’Ni matarajio yetu kupitia mafunzo haya tutakuwa na utumishi uliotukuka kwa kuwa na Watumishi wa Umma wenye kuzingatia weledi na wachapa kazi ili kuendelea kulinda taswira nzuri ya serikali ’’ amesema Mwakilishi wa Katibu Mkuu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika amesema kikao kazi hicho kimewapa fursa ya kubadilishana uzoefu katika nyanja ya usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma pamoja na kujadili mikakati mbalimbali itakayowasaidia kusimamia suala la maadili kwa watumishi wa umma.
"Katika kuhakikisha suala hili linakuwa endelevu tumeweka mikakati ya pamoja kwa lengo la kuhakikisha suala la maadili katika utumishi wa umma linasimamiwa ipasavyo" amesisitiza Bi. Mavika.
Naye Afisa Muuguzi kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Rehema Msanjila amesema mafunzo aliyoyapata yataenda kuleta mapinduzi makubwa katika eneo analolifanyika kazi ikizingatiwa sekta ya afya imekuwa ikilalamikiwa sana katika uvunjifu wa maadili.
“Nina imani kubwa kutokana na mikakati mikubwa
tuliyojiwekea katika kikao hiki, tunakwenda kuwa na wauguzi na madaktari wenye
kuzingatia maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi katika hospitali zetu
hapa nchini’ amesema Bi. Msanjila.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli akizungumza Jijini Dodoma na Maafisa
Waandamizi wakati
akifunga kikao kazi cha siku mbili kilichozikutanisha Taasisi Simamizi
za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora
katika utoaji huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni kutoka Baraza la Ukunga na Maadili Tanzania, Bi. Jane Mazigo akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli baada ya kufunga kikao kazi cha Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Afisa
Muuguzi kutoka Baraza la Ukunga na Maadili Tanzania,
Bi. Rehema Msanjila akielezea faida walizozipata
katika kikao
kazi cha kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma
kwa wananchi
na jinsi
kitakavyoenda
kuleta mapinduzi ya kimkakati.
Friday, June 16, 2023
SERIKALI YAZIDI KUWEKA MIKAKATI KATIKA KUIMARISHA MAADILI KWA WATUMISHI WA UMMA
Na. Lusungu Helela-DODOMA
Tarehe 16 Juni, 2023
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesema itaendelea kuweka mikakati ya kuimarisha uadilifu, uwajibikaji na utawala bora katika Utumishi wa Umma ili kuleta tija iliyokusudiwa kwa maendeleo ya taifa.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Amesema Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama hivyo vya Kitaaluma vina jukumu kubwa la kusimamia dhana ya utawala bora nchini ili kuongeza uwazi na uwajibikaji zaidi katika Utumishi wa Umma katika kuwahudumia wananchi.
"Utawala bora, ni ile dhana inayozingatia maslahi mapana ya taifa, hivyo ninyi Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma muhakikishe huduma mnazozitoa zinazingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji, haki sawa, demokrasia na kuwasikiliza watu wengi na wachache" amesisitiza Bw. Ngangaji.
Amefafanua kuwa, utaratibu wa kuwakutanisha Wataalamu hao kutasaidia kutoa mapendekezo ya namna ya kubadilisha na kuboresha Miongozo ya Usimamizi wa Maadili kwenye Taasisi hizo katika kusimamia dhana ya utawala bora nchini.
Katika hatua nyingine Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu amewataka wasimamizi hao wa maadili kuhakikisha wanawachukulia hatua za kinidhamu watumishi ambao wanakiuka maadili huku akisisitiza kuwapongeza na kuwatia moyo watumishi ambao wanafanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika amesema kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kubaini changamoto za usimamizi wa maadili ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kusimamia maadili kutokana na uzoefu wanaokutana nao.
"Sisi tunaangalia maadili katika masuala ya Utumishi wa Umma lakini kwa wenzetu waliopo kwenye Vyama vya Kitaaluma wanaangalia madili ya kitaaluma kwani wapo Watumishi wa Umma ambao ni wanachama wa vyama hivyo" amesisitiza Bi. Mavika
Akitoa neno la shukrani kwa Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas
Ngangaji, Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Baraza la Uuguzi na
Ukunga, Bi. Jane Mazigo amesema kikao hicho ni muhimu kwao kama wadau muhimu wa
usimamizi na utekelezaji wa maadili ya Utumishi wa Umma katika Vyama vya
Kitaaluma hivyo, anaamini kitatoa mwelekeo mpya katika kuhakikisha
wanabadilishana uzoefu kutokana na
changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Bw.Cosmas Ngangaji akizungumza Jijini Dodoma na Maafisa Waandamizi kwenye kikao kazi kilichozikutanisha Taasisi Simamizi
za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora
katika utoaji huduma kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila
Mavika na upande
wa kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Madilli kutoka Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bi.Leila Mavika akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji kuzungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma kwa lengo
la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Sehemu ya Watumishi Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa
wananchi .
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na maafisa
waandamizi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa
wananchi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Usajili, Maadili na Leseni, Bi. Jane Mazigo akitoa neno
la shukrani kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma, Bw. Cosmas Ngangaji baada ya kuzungumza nao kwenye
kikao kazi na Maafisa Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma
kilicholenga kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa wananchi.
Sehemu ya Watumishi Waandamizi kutoka Taasisi Simamizi za Maadili na Vyama vya Kitaaluma wakiwa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kusimamia dhana ya utawala bora katika utoaji huduma kwa
wananchi.