Sunday, January 26, 2020

URASIMISHAJI ARDHI USHIRIKISHE HALMASHAURI, WIZARA YA ARDHI NA JAMII ILI KUEPUKA MIGOGORO


Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipowasili ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kikazi kukagua miradi ya MKURABITA. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana  na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka.

Mnufaika wa MKURABITA, Bw. Heri Nahala akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na MKURABITA wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kutembelea utekelezaji wa miradi ya MKURABITA katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe .

Friday, January 24, 2020

MHE. MKUCHIKA AKUTANA NA MAKAMISHNA WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KUJADILIANA NAMNA YA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA UTAWALA BORA




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumzia namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora waliomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma.
Baadhi ya Makamishna na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo kuzungumzia namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.
Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Fatuma Muya akitoa maoni yake wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) na Makamishna wa Tume hiyo kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo kilichokuwa na lengo la kujadiliana namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (wa tatu kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora mara baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo kilichokuwa na lengo la kujadiliana namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Mohamed Hamad baada ya kikao na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadiliana namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.

ELIMU YA MANUFAA YA HATIMILIKI ZA KIMILA ITOLEWE KWA WALENGWA WA MKURABITA


Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na  wanakijiji wa Ntandabala kata ya Masoko Wilayani RUNGWE katika ziara ya kikazi ya kukagua mradi wa kurasimisha raslimali za wanyonge ( MKURABITA).

Baadhi ya Wazee na Vijana wa kijiji cha Ntandabala kilichopo Kata ya Masoko Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wakimsikiliza, Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa  alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya uamuzi wa serikali kuanzisha mpango wa kurasimisha raslimali za wanyonge (MKURABITA) na faida zake kwa wanufaika.

Baadhi ya akina Mama wa Kijiji cha Ntandabala kilichopo kata ya Masoko Wilayani Rungwe wakimshukuru  Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa kwa kufanya ziara kijijini hapo na kutoa  maelekezo yatakayowasaidia kutatuliwa kero zao za kurasimishiwa maeneo yao na kunufaika na mikopo katika taasisi za fedha.

Tuesday, January 14, 2020

WAZIRI MKUU AITAKA JAMII KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA VITA DHIDI YA RUSHWA NCHINI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kuzindua ofisi mpya za TAKUKURU zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimkaribisha, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kuzungumza na wananchi mara baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU jana.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) alipokuwa akizungumza nao jana baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana. Kushoto kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi na wa kwanza kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali, John Mbungo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akipanda mti baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na  Usalama ya Mkoa wa Lindi baada ya kuzindua jengo jipya la TAKUKURU lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi jana.


Thursday, January 9, 2020

DKT. MWANJELWA AAGIZA KITENGO CHA MANUNUZI WILAYA YA MKALAMA KICHUNGUZWE KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama katika kikao kazi, kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Emmanuel Luhahula na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Elizabeth Rwegasira (kushoto).
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika kikao kazi kilichofanyika katika  ukumbi wa halmashauri hiyo. 
Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Mhe. Allan Kiula akiwasilisha hoja za watumishi wa jimbo lake wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kilichofanyika leo katika ukumbu wa halmashauri hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tatazi iliyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bw.John Cassiano akiwasilisha hoja kuhusu walimu wanaojiendeleza kielimu kutopandishwa vyeo, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kilichofanyika katika  ukumbi wa halmashauri hiyo 

Wednesday, January 8, 2020

MAAFISA TARAFA NCHINI WATAKIWA KUSHIRIKI VIKAO VYA KAMATI ZA KUDUMU NA BARAZA LA MADIWANI ILI KUSIMAMIA VYEMA SHUGHULI ZA MAENDELEO


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba katika ziara yake ya kikazi, mkoani Singida.

Baadhi ya watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika ziara yake ya kikazi mkoanI Singida. 
Afisa Mtendaji Kata ya Tulya, Bi. Mwajuma Rugambwa akiwasilisha malalamiko yake wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri mkoani Singida.