Monday, March 19, 2018

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA TAASISI ZAKE KWA KUTEKELEZA VIZURI MAJUKUMU KATIKA MWAKA WA FEDHA 2017/18

Add caption

Add caption

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akifungua kikao cha kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI  iliyowasilishwa kwenye kamati  hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Selasini (Mb) akichangia hoja kuhusu Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI  iliyowasilishwa kwenye kamati  hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa.

No comments:

Post a Comment