Saturday, March 17, 2018

WANANCHI WILAYANI MASWA WANUFAIKA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI

Add caption

Add caption

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akimkabidhi  mnufaika  wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Bi. Monica Kwilasa msaada wa pesa zilizochangwa na wajumbe wa kamati yake ikiwa ni sehemu ya kumpongeza mnufaika huyo kwa kujenga nyumba kupitia pesa za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini zinazotolewa na TASAF.


Wanafunzi wa shule ya Nyalikungu Sekondari wilayani Maswa ambao ni wanufaika wa pesa za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wakitoa burudani kwa wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi  inayotekelezwa na TASAF.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne A. Sagini  akiwakaribisha  Wilayani Maswa  wajumbe  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi  inayotekelezwa na TASAF mkoani Simiyu.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Maswa wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi  inayotekelezwa na TASAF.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakijitambulisha kwa wananchi wilayani Maswa wakati wa ziara yao ya kikazi ya kukagua maendeleo ya miradi  inayotekelezwa na TASAF.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akizungumza na wananchi wilayani Maswa wakati wa ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na TASAF.

No comments:

Post a Comment