Baadhi ya watumishi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini yaliyokua yakiendelea wakati wa ziara ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke leo Jijini Dar es Salaam kuhitimisha wiki ya utumishi wa umma iliyofanyika tarehe 16 hadi 23 Juni, 2017 na kupokea taarifa ya wilaya pamoja na kero za watumishi. |
Watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Temeke
wametakiwa kuzingatia mkataba wa huduma kwa mteja pale wanapohudumia wateja na
kushughulikia kero za wananchi kwa wakati ili waweze kuendana na kasi ya
serikali ya awamu ya tano.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J.
Kairuki wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke katika
kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma iliyofanyika tarehe 16 hadi 23 Juni, 2017
na kupokea taarifa ya wilaya hiyo pamoja na kero za watumishi leo Jijini Dar es
Salaam.
Katika kuboresha maslahi ya watumishi Mhe.
Kairuki ametoa wito kwa waajiri kurekebishe taarifa za watumishi wote
waliokaribia kustaafu na wale ambao wamepandishwa vyeo bila kulipwa stahili zoa
ili waweze kulipwa stahili hizo kabla ya kustaafu, huku akiwataka wale
waliokwisha staafu wakiwa na barua za kupandishwa vyeo kujaza fomu kupitia kwa
waajiri wao ili waweze kupata stahili zoa kwani hakuna haki na stahili ya
mtumishi wa umma itakayopotea.
Aidha mhe. Kairuki amewataka watumishi
wote wa umma kujisajiri katika tovuti ya watumishi (watumishi portal) ili wawe
na uwezo wa kuona taarifa zao za kiutumishi na kuweza kufuatilia masuala yao ya
kiutumishi yamefikia katika hatua gani.
“Maafisa utumishi na ofisi ya katibu
tawala hakikisheni kuwa taarifa zote za kwenye mfumo zinakua ni taarifa safi na
zilizo kamilika kwa kuhakikisha kwamba watumishi wana tarehe kamili na sahihi
za kuzaliwa, tarehe zao za ajira, tarehe zao za kila mara walipopandishwa vyeo,
taarifa zao za mifuko kwenye hifadhi ya majii, sifa zao za kielimu, vyeo
walivyonavyo pamoja na masuala mengine” Amesema Mhe. Kairuki
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Mhe. Felix J. Lyaniva amemhakikishia Mhe.
Kairuki kuwa Halmashauri yake imejitahidi kusimamia kwa karibu watendaji
wake jambo ambalo limeboresha utoaji wa huduma kwa wateja kwa wakati lakini pia
kuhakikisha kuwa watumishi wake wanafiki ofisini mapema kwa kuwahamasisha
kuishi maeneo ya karibu na kituo chao cha kazi.
Akichangia mada wakati wa ziara hiyo
Mwalimu Mkuu kutoka shule ya Msingi Yombo Dovya Bw. Godwin Jerome Mselle
amemuomba Mhe. Kairuki kuangalia namna ambavyo walimu wote watakavyowezeshwa
kupata mafunzo kazini ili waweze kwenda sambamba na mitaala mipya tofauti na inavyofanywa
kwa sasa kwa kupeleka walimu wachache kupata mafunzo hayo na kuja kufundisha
walimu wengine jambo ambalo halifanywi kwa ufasaha kama ambavyo walimu wote
wangepata mafunzo hayo kwa pamoja kutoka kwa wataalamu.
No comments:
Post a Comment