Friday, July 14, 2017

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MFUMO WA HCIMS ILI UWEZE KUTUMIKA NA WATUMISHI WENGI ZAIDI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe (hawapo pichani) leo alipofanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma Jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mhudumu wa Afya kutoka Hospitali ya Magomeni Bii. Rukia Mkapa akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mwalimu Paschal Mugayana kutoka shule ya Sekondari ya Njechele akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



1 comment: