Thursday, July 20, 2017

Mhe.Kairuki akutana na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es Salaam


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Segerea alipofanya ziara ya kikazi  ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo akiwatambulisha baadhi ya watumishi na viongozi wa Segerea waliohudhuria kikao kazi kilichowakutanisha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) Jijini Dar es Salaam. 


Meneja Masoko kutoka kampuni ya Watumishi (Watumishi Housing Company), Bw. Raphael Mwabuponde, akiwasilisha mada kuhusu taratibu za kupata nyumba kwa Watumishi wa Umma wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na Watumishi wa Umma wa Segerea, Jijini Dar es Salaam.

Mkazi wa Segerea, Bw. Juma Kali akiwasilisha hoja maalum wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala - Segerea  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Sala

   Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mhe. Bonnah Kaluwa akitoa salamu wakati wa kikao kazi na kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), leo Jijini Dar es Salaam. 


Mtumishi wa Umma kutoka Tabora, Bw. John Joseph akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kutoka Segerea na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam. 



No comments:

Post a Comment