Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki
(Mb) akisisitiza juu ya ukamilishaji wa zoezi la usajili wa watumishi wa umma
mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo mkoani humo, aliyoifanya
kwa lengo la kufanya tathmini ya zoezi
hilo . Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella akimsikiliza.
|
mheshimiwa waziri nakupongeza kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya kwa ajiri ya kuboresha utumishi wa umma.
ReplyDeleteLakini kuna swala naona haliwekwi sawa pamoja na mamlaka kua ikitoa ufafanuzi, ni kuhusiana na sisi tuliositishiwa ajira na kurudishwa nyumbani kupisha zoezi hilo, serikali ipo kimya na haisemi ni lini tutarudishwa kazini takribani miezi minne imepita hatujui muafaka wetu. Tunakuomba sana mheshimiwa waziri tusaidie kuokoa maisha yetu sisi vijana tulio tayari kutumikia taifa letu katika utumishi wa umma, tunaomba kurudishwa kazini