Tuesday, July 2, 2019

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA UTUMISHI WA UMMA KWA MARA YA KWANZA, DKT. MWANJELWA AIWAKILISHA TANZANIA BARA KATIKA MAADHIMISHO HAYO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein, akifungua kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar, iliyofanyika kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein, akifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akiagana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) baada ya kumalizika kwa  kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma Zanzibar, liliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment