Monday, September 26, 2016
Sunday, September 25, 2016
LIJUE GAZETI LA SERIKALI
GAZETI LA SERIKALI-sehemu iliyopita tuliona matumizi ya taarifa zinazochapishwa katika gazeti la serikali ikiwamo kufuatilia masuala mbalimbali ya kisheria, na aina ya taarifa hizo.
Leo tunaangalia lugha inayotumika katika Gazeti la Serikali, bila shaka umewahi kujiuliza kuhusu jambo hili. Lugha inayotumika katika taarifa za Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Kanuni C. {2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la 2009 na Establishment Circular letter No. 7 ya mwaka 1970, taarifa zote zinatakiwa kuwa katika lugha ya Kiswahili isipokuwa taarifa zinazohusu matangazo ya Kisheria, kwa maana ya Miswada ya Bunge na matangazo ya Serikali, Government Notice, ambayo hutangazwa kwa lugha ya Kiingereza.
https://www.facebook.com/utumishiweek
Gazeti la Serikali hupatikana wapi?, itaendelea..
MHE. KAIRUKI AWATAKA WAAJIRI WOTE SERIKALINI KUHAKIKISHA KUWA WATUMISHI WALIO KATIKA MAMLAKA ZAO WANASAJILIWA KWA AJILI YA KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA NDANI YA SIKU 14, NA KUWASILISHA TAARIFA YA ZOEZI HILO OFISI YA RAIS-UTUMISHI. SERIKALI IMEPANGA KUFANYA ZOEZI HILO LA USAJILI NA UTOAJI WA UTAMBULISHO NA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WATUMISHI WA UMMA WOTE KUANZA TAREHE 03 OKTOBA, 2016.
Subscribe to:
Posts (Atom)