Thursday, October 23, 2014
Friday, October 17, 2014
KLABU YA MICHEZO YA UTUMISHI YAKABIDHI VIKOMBE KWA WAZIRI KOMBANI
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akitoa mkono wa
pongezi kwa Timu ya mpira wa pete ya Utumishi katika hafla fupi iliyofanyika
ofisini kwake.
|
Wednesday, October 15, 2014
UTUMISHI BINGWA MPYA MPIRA WA PETE SHIMIWI 2014
Wachezaji wa Ofisi ya Rais Utumishi wakiwa katika maandamano huku wakipunga
mkono kwa mgeni rasmi siku ya kilele cha mashindano ya SHIMIWI 2014 uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
|
Timu ya mpira wa Pete ya
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa kwa
Mashindano ya 38 ya SHIMIWI kwa mwaka 2014.
Utumishi imefanikiwa kuwa
bingwa baada ya kuisambaratisha timu Wizara ya Afya kwa ushindi mnono wa Pete 65
kwa 35 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Katika mchezo huo, wachezaji
Fatuma Machenga (GS) na Anna Msulwa (GA) wa Utumishi wakicheza kwa ushirikiano
waliliongoza jahazi la Utumishi na kufanikisha ushindi huo mnono. Machenga (GS)
alifanikiwa kufunga 45 na Msulwa (GA) 20 hivyo kuhakikisha Utumishi inakua
bingwa.
Mara baada ya mchezo
kumalizika, kocha wa timu ya Afya Mwajuma Kisengo alisema mchezo ulikuwa mzuri
na wenye ushindani ila bahati haikua yao na wanasubiri mashindano yajayo.
“Mimi kama kocha na mwamuzi
wa kimataifa nawapongeza wachezaji wangu na wenzao wa Utumishi, pamoja na
waamuzi ambao wamechezesha vizuri kwa kuzingatia sheria za mchezo huu” Kisengo alisema.
Naye kocha wa Utumishi Bw.
Methew Kambona aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kunyakua kombe
la SHIMIWI 2014.
Utumishi ilifuzu hatua ya
fainali baada ya kuifungashia virago Ikulu ambao walikuwa mabingwa watetezi kwa
jumla ya magoli 42 dhidi ya 41 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa jana katika
uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Saturday, October 11, 2014
OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NDIO MABINGWA WA MPIRA WA PETE SHIMIWI 2014
Hekaheka ya kuwania mpira
baina ya wachezaji wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za
kijani) na Afya katika mechi ya fainali ya SHIMIWI 2014 iliyochezwa uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
|
Mashabiki wa timu ya mpira
wa pete ya Ofisi ya Rais,Utumishi wakiishangilia timu yao wakati wa fainali
iliyoikutanisha timu yao na Afya katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.
|
Baadhi ya washabiki wa mchezo
wa mpira wa pete wakishuhudia fainali kati ya Utumishi na Afya wakati wa mchezo
uliozikutanisha timu hizo katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)