Wednesday, December 31, 2014
Monday, December 15, 2014
WATAALAMU 12 WA KUJITOLEA KUTOKA NCHINI JAPANI WAMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI
Mtalaamu wa kujitolea Bw.Keisuke Yamamoto akitoa mada wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalamu wa kujitolea kutoka Japani iliyofanyika Utumishi. |
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.Mick Kiliba (kushoto) akimpongeza mmoja kati ya watalaam wa kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Keisuke Yamamoto baada ya kumaliza muda wa kujitolea nchini. |
Thursday, December 11, 2014
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili ya Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. Mathew Kirama akitoa maoni katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya hali ya maadili katika Utumishi wa Umma. |
Mtaalamu mwelekezi toka Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Francis
Mwaijande (wa pili toka kushoto) akiwasilisha matokeo ya utafiti juu ya hali ya
uzingatiaji wa maadili katika Utumishi wa Umma.
|
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa
kwanza kulia) akizungumza katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya
hali ya uzingatiaji wa maadili katika Utumishi wa Umma.
|
Wednesday, November 26, 2014
Monday, November 17, 2014
UBALOZI WA INDIA WAADHIMISHA MIAKA 50 YA MPANGO WA USHIRIKIANO WA KIUFUNDI NA UCHUMI WA SERIKALI YA INDIA (ITEC)
Thursday, October 23, 2014
UTUMISHI YAFANYA KIKAO KAZI KWA VIDEO CONFERENCE NA MIKOA YA SINGIDA,ARUSHA,DODOMA NA TUME YA MIPANGO
Friday, October 17, 2014
KLABU YA MICHEZO YA UTUMISHI YAKABIDHI VIKOMBE KWA WAZIRI KOMBANI
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akitoa mkono wa
pongezi kwa Timu ya mpira wa pete ya Utumishi katika hafla fupi iliyofanyika
ofisini kwake.
|
Wednesday, October 15, 2014
UTUMISHI BINGWA MPYA MPIRA WA PETE SHIMIWI 2014
Wachezaji wa Ofisi ya Rais Utumishi wakiwa katika maandamano huku wakipunga
mkono kwa mgeni rasmi siku ya kilele cha mashindano ya SHIMIWI 2014 uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
|
Timu ya mpira wa Pete ya
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa kwa
Mashindano ya 38 ya SHIMIWI kwa mwaka 2014.
Utumishi imefanikiwa kuwa
bingwa baada ya kuisambaratisha timu Wizara ya Afya kwa ushindi mnono wa Pete 65
kwa 35 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Katika mchezo huo, wachezaji
Fatuma Machenga (GS) na Anna Msulwa (GA) wa Utumishi wakicheza kwa ushirikiano
waliliongoza jahazi la Utumishi na kufanikisha ushindi huo mnono. Machenga (GS)
alifanikiwa kufunga 45 na Msulwa (GA) 20 hivyo kuhakikisha Utumishi inakua
bingwa.
Mara baada ya mchezo
kumalizika, kocha wa timu ya Afya Mwajuma Kisengo alisema mchezo ulikuwa mzuri
na wenye ushindani ila bahati haikua yao na wanasubiri mashindano yajayo.
“Mimi kama kocha na mwamuzi
wa kimataifa nawapongeza wachezaji wangu na wenzao wa Utumishi, pamoja na
waamuzi ambao wamechezesha vizuri kwa kuzingatia sheria za mchezo huu” Kisengo alisema.
Naye kocha wa Utumishi Bw.
Methew Kambona aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kunyakua kombe
la SHIMIWI 2014.
Utumishi ilifuzu hatua ya
fainali baada ya kuifungashia virago Ikulu ambao walikuwa mabingwa watetezi kwa
jumla ya magoli 42 dhidi ya 41 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa jana katika
uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Saturday, October 11, 2014
OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NDIO MABINGWA WA MPIRA WA PETE SHIMIWI 2014
Hekaheka ya kuwania mpira
baina ya wachezaji wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za
kijani) na Afya katika mechi ya fainali ya SHIMIWI 2014 iliyochezwa uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
|
Mashabiki wa timu ya mpira
wa pete ya Ofisi ya Rais,Utumishi wakiishangilia timu yao wakati wa fainali
iliyoikutanisha timu yao na Afya katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.
|
Baadhi ya washabiki wa mchezo
wa mpira wa pete wakishuhudia fainali kati ya Utumishi na Afya wakati wa mchezo
uliozikutanisha timu hizo katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)