Wednesday, December 31, 2025
Wednesday, December 24, 2025
Monday, December 15, 2025
MKOMI ATOA WITO KWA WATUMISHI KUJICHUNGUZA KAMA WANAFAA KUWA VIONGOZI
Na.Mwandishi Wetu
Tarehe 15 Disemba, 2025
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Bw. Juma Mkomi amesema kuwa mtumishi wa umma anaweza kujifanyia uchunguzi (vetting)
mwenyewe juu ya tabia na mwenendo katika utendaji kazi bila kusubiri taarifa ya
vyombo vya usalama.
Bw. Mkomi
alisema hayo Desemba 15, 2025 kwa Watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa kuhitimisha
mafunzo ya uelewa wa namna bora ya kulinda taswira nzuri ya taasisi yaliyofanyika
Mtumba jijini Dodoma.
“Mtumishi anaweza kujichunguza na kuona kama anafaa kuwa kiongozi
au la, kwa sababu tabia njema au mbaya anaweza kuitambua kwa ufasaha mtumishi
mwenyewe” alisema Bw. Mkomi.
Bw. Mkomi aliongeza kuwa tabia na mienendo ya watumishi
inatakiwa kuwa na taswira chanya kwao wenyewe na mbele ya macho ya wale
wanaopokea huduma kutoka kwao.
Aidha, Bw. Mkomi alisisitiza kuwa tabia na mienendo ya
watumishi wa ofisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na misingi mikuu ya utendaji
kazi wa ofisi, pia tabia hizo zitoe mitazamo chanya juu ya utendaji kazi wao na
namna anavyowahudumia watumishi wa umma na umma kwa jumla.
Awali, Mkufunzi Bw. Moses Raymond alisema kuwa Watumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI ni kioo kwa
watumishi wengine wote katika utumishi wa umma na ndio wenye dhamana ya kusimamia
utumishi wa umma nchini. Hivyo, hawana budi kuwaongoza watumishi wengine vyema katika
ujenzi wa taswira chanya ya Serikali.
Alifafanua kuwa, mtumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI akifanya
vibaya katika utoaji wa huduma, wananchi wanatafsiri kuwa watumishi wote wa
ofisi hiyo wana tabia hiyo.
“Binafsi natoa rai katika mafunzo haya kuhakikisha kila mmoja anashiriki ipasavyo katika jitihada
za ujenzi wa taswira nzuri ya ofisi kwa kufanya vyema hususani katika
utekelezaji wa majukumu yake ili kulinda taswira chanya ya ofisi” aliongeza Bw.
Raymond.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa
mafunzo ya uelewa yanayofanyika
kila Jumatatu ya Wiki katika Ofisi hiyo Mtumba
jijini Dodoma tarehe 15 Desemba,
2025.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.
Juma Mkomi (Kulia) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Xavier Daudi wakifuatilia mada kuhusu namna bora ya kulinda
taswira nzuri ya taasisi wakati wa mafunzo ya uelewa yanaliyofanyika katika Ofisi
hiyo Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Desemba, 2025.
Viongozi
na Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
wakifuatilia mada kuhusu namna bora ya kulinda taswira nzuri ya taasisi kutoka
kwa Mkufunzi Moses Raymond wakati wa mafunzo ya uelewa yaliyofanyika katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Desemba,
2025.
Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mada kuhusu namna bora ya kulinda taswira nzuri ya taasisi kutoka kwa Mkufunzi Moses Raymond wakati wa mafunzo ya uelewa yaliyofanyika katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Desemba, 2025.
Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mada kuhusu namna bora ya kulinda taswira nzuri ya taasisi kutoka kwa Mkufunzi Moses Raymond wakati wa mafunzo ya uelewa yaliyofanyika katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Desemba, 2025.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Nyasinde Mkono akitoa neno la shukurani baada ya mafunzo ya namna bora ya kulinda taswira nzuri ya taasisi yaliyofanyika katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Desemba, 2025.
Saturday, December 13, 2025
MATUKIO YA PICHA LEO DISEMBA 13, 2025 IKIWA KATIKA IBADA MAALUM YA KUAGA MWILI WA ALIYEWAHI KUWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS - UTUMISHI MAREHEMU JENISTA MHAGAMA JIJINI DODOMA
![]() |
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi akishiriki ibada
maalum ya kuuaga mwili wa Marehemu Mhe
Jenista Mhagama ambaye aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – UTUMISHI
leo 13/12/2025 Jijini Dodoma. |
![]() |
Mkurugenzi wa Mishahara Malupulupu
na Maslahi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.
Mariam Mwanilwa (Kulia) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Bajeti ofisi
hiyo Bi. Julieth Magambo (Kushoto) wakishiriki Misa ya Kuuga mwili wa aliyewahi
kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – UTUMISHI Mhe Jenista Mhagama Leo tarehe
13/12/2025 katika Parokia ya Kiwanja Cha Ndege Jijini Dodoma. |
WAZIRI KIKWETE AAHIDI USHIRIKIANO KWA WATUMISHI WA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI
Na. Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameipongeza
Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa kuongoza
na kusimamia Ndege za Serikali kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Waziri Kikwete amesema hayo Desemba 12, 2025 jijini Dar es salaam
wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa lengo la
kujitambulisha.
“Ninaipongeza Bodi kwa kuendelea kuwa washauri wazuri na kufanya uendelevu wa
Wakala, binafsi ninaridhika na utendaji kazi wake. Pia Nitumie fursa hii
kuwapongeza watumishi wote kwa ustadi wenu mkubwa wa kusimamia Ndege za
Serikali, mimi na Naibu Waziri wa ofisi yangu Mhe. Regina Qwaray
tunawahakikishia ushirikiano wa dhati wakati wote wa uongozi wetu” alisema Mhe.
Kikwete.
Aidha,
Mhe. Kikwete amewapongeza kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ambao
unaonekana kuridhisha viongozi wanawahudumia. Hivyo, ametoa rai pia kwa
watumishi hao kumpa ushirikiano Naibu Waziri Mhe. Regina Qwaray kwa kuwa
anamfahamu uwezo wake katika kazi na atasaidia kuongeza ufanisi mara dufu.
Vile
vile Mhe. Kikwete amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuongoza Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo TGFA ni moja ya
taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo.
Naye,
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray
ameahidi kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya taasisi hiyo muhimu
katika Taifa.
“Leo tumekuja kujitambulisha ili tupate kufahamiana kwa kuwa sisi ndio tutafanya kazi pamoja, naomba tuendelee kuwa na ari ile ile ya kufanya kazi kwa ushirikiano ili tuweze kufanikiwa” alisema Mhe. Qwaray.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali Capt. Budodi
Nicholaus Budodi alisema kuwa Wakala inaendelea vizuri kusimamia miradi
mbalimbali inayoendelea katika ofisi hiyo.
Vile vile, kwa niaba ya taasisi ameahidi kuendelea kuwa wasikivu katika maelekezo wanapata kutoka kwa viongozi na kutekeleza kwa wakati na kwa ufanisi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti na
Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea
ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za
Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (aliyesimama) akisoma taarifa ya taasisi hiyo pamoja na
maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala ya Ndege za Serikali wakati Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali
(TGFA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati
Waziri huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi Idrissa
Mshoro
(kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri
huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
(wapili kutoka kushoto) akielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala wa Ndege za
Serikali jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu
Waziri wa Ofisi yake Mhe. Regina Qwaray. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za
Serikali (TGFA), Capt. Budodi
Budodi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wakwanza kushoto)
akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (wakwanza kulia). Wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina
Qwaray na wa pili kutoka kushoto
ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za
Serikali, Prof. Mhandisi Idrissa Mshoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia)
akifurahia jambo kabla ya kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya
Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni
Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Regina Qwaray.
Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (wakwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wapili kutoka kushoto). Wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia)
akiwasili katika ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea
ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kabla ya kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Regina Qwaray.
Sehemu ya Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali
(TGFA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri
huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali
(TGFA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati
Waziri huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina
Qwaray (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi Idrissa
Mshoro. Katikati ni Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akisalimiana na Viongozi, Watendaji na Watumishi
wa Wakala ya
Ndege za Serikali baada ya kuwasili katika ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Watumishi na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) baada ya
kuzungumza nao alipokwenda kujitambulisha katika ofisi hiyo jijini Dar es
Salaam
Friday, December 12, 2025
SERIKALI KUJENGA UTUMISHI WA UMMA WENYE UFANISI, UWAJIBIKAJI NA KUONGEZA FURSA ZA AJIRA NA USTAWI WA VIJANA
Na Veonica Mwafisi-Dar es Salaam
Tarehe 12 Disemba, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali kupitia Ofisi yake inaonesha dhamira
thabiti ya kujenga Utumishi wa Umma wenye ufanisi, uwajibikaji na unaozingatia
misingi ya utawala bora ili kwenda sambamba na matarajio ya Dira ya Maendeleo
ya Taifa ya 2050.
Waziri Kikwete amesema hayo wakati wa Mkutano wake na
Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es
salaam Desemba 12, 2025. Mkutano huo ulilenga kutoa taarifa ya namna Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inavyotekeleza wajibu
wake kwa Taasisi za umma, Watumishi wa Umma na Wananchi kwa jumla.
Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, dhamira hiyo imeweka
vipaumbele ambavyo ni kuongeza fursa za ajira na ustawi wa vijana wa
kitanzania, maboresho ya mifumo ya ajira, utoaji wa huduma, mafunzo ya kujenga
uwezo, usimamizi wa rasilimaliwatu pamoja na kuimarisha mifumo ya mawasiliano kati
ya Serikali na wananchi.
Mhe. Kikwete alibainisha kuwa Serikali inaendelea
kuhakikisha nafasi za ajira katika Utumishi wa Umma zinakuwa za wazi na
ushindani kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ili
kuwajengea Watanzania imani na uaminifu kwa Serikali yao kwa ustawi wa Taifa.
Vile vile, Mhe. Kikwete amesema, kupitia Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2050 imeelekeza Sekta ya kipaumbele iwe na uwezo wa kuzalisha ajira
na kuongeza fursa ya ajira kwa vijana, kuongeza kipato kwa wananchi na
kupunguza umaskini kwa kuzingatia viwango vya juu vya weledi unaopatikana na
kufuata misingi ya haki, umahiri na utendaji bora.
Aidha, Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, katika kufanikisha
maelekezo ya Dira 2050, kupitia Serikali kwa mwaka wa Fedha 2025/26 kibali cha
nafasi 41,500 za ajira zikiwemo nafasi 12,000 za ajira ambazo ni ahadi ya Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoahidi kutoa nafasi 5,000 za kada
za Afya na nafasi 7,000 za Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati ambazo ni
uzalishaji wa ajira zilizo rasmi ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani.
Mhe. Kikwete amesema kuwa, ili kuhakikisha usaili
unafanyika kwa wakati na kwa lengo la kuongeza ufanisi, usaili wa mchujo wa
nafasi hizo utafanyika kwa kutumia mfumo wa kieletroniki uitwao “Online
Aptitude Test (OATS)” na utafanyika katika vituo mbalimbali kama vile Taasisi
za Elimu ya Juu, Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi (VETA) na Shule za
Sekondari zenye maabara za Komputa zinazopatikana katika mikoa yote na Vituo
mahsusi kwa Unguja na Pemba.
“Mhe. Rais Dkt. Samia aliahidi baada ya kuingia madarakani
atatoa nafasi 5,000 za kada za Afya na nafasi 7,000 za Walimu ndani ya siku 100
na tayari nafasi za ajira 12,000 zimeshatangazwa na waombaji wenye sifa
wameitwa kwenye usaili utakaofanyika kuanzia tarehe 13 Desemba, 2025 katika
mikoa yote Tanzania Bara na Vituo mahsusi kwa Unguja na Pemba,” Amefafanua Mhe.
Kikwete.
Pia, Waziri huyo aliwaomba wandishi wa habari kuendelea
kuwahabarisha na kuwaelimisha Watanzania hususan vijana, kutambua fursa
zilizopo na kuzitumia kwa manufaa ya taifa. Utambuzi huo unaifanya Serikali kuendelea
na jitihada zake za kukuza ujuzi, kuhimiza maadili, kupanua fursa za makazi
bora na kuandaa vijana wa Kitanzania ili kukabiliana na uchumi wa kidijiti.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waandishi
wa Habari (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wake na Waandishi hao
uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi
yake.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo kwenye Mkutano
wake na Waandishi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es
salaam. Wa kwanza kulia waliokaa ni Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray. Wengine ni
Viongozi na Watendaji wa Ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wanne kutoka kushoto) akimsikiliza, Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa (hayupo pichani) alipokuwa
akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza na
Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI. Watatu
kutoka kushoto ni Naibu Waziri, wa Ofisi
yake Mhe. Regina
Qwaray na wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ofisi yake Mhe. Regina Qwaray (kushoto) kabla ya kuanza kwa
Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa
Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam kwa
lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake.
Mwandishi wa Habari kutoka Kituo cha Habari Azam Tv, Bi. Sheila Mkumba
(aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo
jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya
ofisi yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (kulia) kabla ya Waziri huyo
kuzungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wake na Waandishi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Habari
Maelezo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu
ya ofisi yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyesimama kulia) akizungumza na Waandishi wa
Habari wakati wa Mkutano wake na Waandishi hao
uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam uliolenga
kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake. Wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa
Ofisi yake Mhe. Regina Qwaray. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi hiyo.
Mwandishi wa Habari kutoka Kituo cha Habari Radio Maria, Bw. Martin Joseph
(aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo
jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya
ofisi yake.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo kwenye Mkutano
wake na Waandishi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es
salaam. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi yake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Regina Qwaray (watatu kutoka
kushoto) akifuatilia Mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam
uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake.
Thursday, December 11, 2025
MHE. RIDHIWANI KIKWETE AWAKUMBUSHA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUZINGATIA WAJIBU WAO WA KUSIMAMIA MAADILI BILA UPENDELEO
Na Antonia Mbwambo na Eric Amani-Dodoma
Tarehe 11 Disemba, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
– UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ametoa wito kwa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhakikisha inatekeleza majukumu
yake kwa weledi, uadilifu na bila upendeleo kwa kiongozi yeyote.
Akizungumza wakati
akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu
Nchemba kwa ajili ya kuzungumza na watendaji wa Sekretarieti hiyo, Mhe. Kikwete
amesisitiza umuhimu wa chombo hicho katika kusimamia maadili kwa kuzingatia
misingi ya sheria, uwazi, ukweli na usawa, ili kuendelea kujenga taswira njema
ya utumishi wa umma nchini.
Ameeleza kuwa viongozi wa umma
wana wajibu mkubwa kwa jamii, hivyo ni muhimu Sekretarieti hiyo kutekeleza
dhima yake ya kisheria ya kuhakikisha viongozi wote wanazingatia miiko na
maadili katika kutekeleza majukumu yao.
“Hatuwezi kuwa na Serikali
ambayo viongozi wanalalamikiwa kwamba ni wapotofu wa Maadili na sisi kama
chombo cha kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma tumekaa kimya” Waziri Kikwete
alisema.
Aidha, ametoa rai kwa
watumishi wa Sekretarieti ya Maadili kuimarisha ushirikiano, kuendesha
uchunguzi kwa haki bila upendeleo na kutoa elimu ya kutosha kuhusu maadili kwa
viongozi wa umma na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wao, watendaji wa Sekretarieti hiyo wamemhakikishia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – UTUMISHI Mhe. Ridhiwani Kikwete kuwa wataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia uwajibikaji, uadilifu na weledi ili kuimarisha imani ya wananchi katika mifumo ya utawala bora
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na menejimenti na watumishi wa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Ofisi hiyo leo tarehe Disemba 11, 2025 Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete na Kushoto ni Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka wakati wakimsubiria Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba awasili katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) baada ya kuwasili katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo Disemba 11, 2025.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Maadili,Jaji Mstaafu Bw. Sivangilwa Mwangesi (katikati) pamoja na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka (kulia) wakati wakimsubiria Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuwasili katika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa ziara ya kikazi iliyofanyika leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.
1. Waziri Mkuu wa Jamhurin ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba akiwasili katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo Disemba 11, 2025
.png)
.png)












.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)