Na. Veronica Mwafisi
Tarehe 10 Februari, 2025-Morogoro
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu amesema mafunzo yanayotolewa kwa Washiriki kutoka Serikali Kuu zikiwemo (Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali), Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko yataongeza ufanisi katika utoaji haki kwenye Utumishi wa Umma.
Mhe.
Sangu amesema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya
Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Mhe. Sangu amesema kuwa, kutokana na Serikali
kusisitiza matumizi ya mifumo kwenye utendaji wa shughuli zake, Tume
ya Utumishi wa Umma, imejenga Mfumo wa kushughulikia Rufaa na Malalamiko kwa
Watumishi wa Umma, Mamlaka za Rufaa, Mamlaka za Nidhamu na Waajiri kwa
lengo la kutoa huduma bora ili kuendana na Serikali ya kidijitali inayoongozwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe.
Sangu ameongeza kuwa mfumo huo utasaidia kupatikana
kwa taarifa za hali ya Utumishi wa Umma kwa
wakati na katika ubora unaotakiwa kulingana na uzito wa taarifa hizo.
Naibu Waziri Sangu
amewasihi washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema Mfumo huo na kuhakikisha wanatuma taarifa sahihi Tume ya
Utumishi wa Umma
kwa lengo la kuchakatwa na kuwasilisha taarifa hizo kwa Mamlaka
husika ili kuirahisishia Serikali
kupanga masuala mbalimbali yanayohusu Utumishi wa Umma.
Aidha, Naibu Waziri Sangu amewataka Waajiri, Mamlaka za Ajira na
Mamlaka za Nidhamu
kuwasilisha vielelezo vya rufaa na malalamiko Tume ya
Utumishi wa Umma
kwa wakati kama Sheria inavyoelekeza pale zinapotakiwa kufanya hivyo.
Kwa
Upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma
Mhe.
Hamisa Kalombola (Jaji Mst), amesema kuwa Tume iliamua kujenga mifumo
ya kielektroniki na kuendelea kutoa elimu ya kutumia mifumo hiyo kwa wadau wao
ili kuondokana na baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinakwamisha utendaji
kazi wa namna ya kuitumia wakati wa uendeshaji wa mashauri na nidhamu hasa
kwenye ushughulikiaji wa rufaa na malalamiko.
Awali, Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma
Bw. John Mbisso alisema, mafunzo hayo yanafanyika
ili kutekeleza Sheria ya Utumishi wa Umma ya kutoa miongozo na elimu ya masuala
mbalimbali ya kiutumishi kwa lengo la kuboresha usimamizi wa Watumishi wa Umma.
Tume
ya Utumishi wa Umma ni chombo rekebu chini ya Ofisi ya Rais kilichoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1)
cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 [Marejeo ya Mwaka 2019].
Aidha,
majukumu ya Tume yameainishwa katika Kifungu cha 10(1) cha Sheria hiyo ambapo
baadhi ya majukumu yake ni pamoja na kutoa Miongozo, Uwezeshaji, Utafiti,
kufuatilia Uzingatiaji katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma na ushughulikiaji
wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa
na Malalamiko katika Utumishi wa Umma yanayofanyika mkoani Morogoro.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo kuhusu Mfumo wa
ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) wakati akifungua
mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa
Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. Hamisa Kalombola (Jaji Mst) akitoa neno
la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo kuhusu Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na
Malalamiko katika Utumishi wa Umma yanayofanyika mkoani Morogoro.
Sehemu ya Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mafunzo waliyoyaratibu kuhusu Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma yanayofanyika mkoani Morogoro.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo kuhusu Mfumo
wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma wakifuatilia
mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Morogoro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (wapili kutoka kulia) akiagana na Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. John Mbisso (kulia) wakati akiondoka baada ya kufungua mafunzo kuhusu Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma yanayofanyika mkoani Morogoro. Aliyejitanda kilemba ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. Hamisa Kalombola (Jaji Mst). Nyuma yake ni Naibu Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bi. Celina Maongezi.
Mkurugenzi wa Idara ya Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti, Bw. Peleleja Masesa akitoa utambulisho wa washiriki waliohudhuria mafunzo kuhusu Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma yanayofanyika mkoani Morogoro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (katikati)
akifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko
katika Utumishi wa Umma yanayofanyika
mkoani Morogoro. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. Hamisa Kalombola (Jaji Mst).
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma na Washiriki kutoka Serikali Kuu zikiwemo (Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali), Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya kufungua mafunzo kuhusu Mfumo wa ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma yanayofanyika mkoani Morogoro.
Afisa
Utumishi, Bodi ya Pamba Tanzania ambaye ni mshiriki wa Mafunzo ya Mfumo wa ushughulikiaji
wa Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma Bi. Changwa Mkwazu akitoa neno
la shukrani kwa niaba ya washiriki wote kwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (hayupo
pichani) baada ya Waziri huyo kufungua mafunzo hayo yanayofanyika mkoani
Morogoro.