Tuesday, April 4, 2023

MHE. SIMBACHAWENE ADHAMIRIA KUSIMAMIA WATUMISHI WA UMMA KUTUMIA VEMA SAA ZA KAZI KUWAHUDUMIA WANANCHI

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 04 Aprili, 2023 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameeleza dhamira yake ya kushirikiana na watumishi wa ofisi yake katika kutekeleza jukumu la kuwasimamia watumishi wa umma nchini kutumia vizuri saa za kazi kuwahudumia wananchi badala ya kufanya mambo ambayo yanakwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi. 

Mhe. Simbachawene ameweka wazi dhamira hiyo ya kuwasimamia watumishi wa umma kutekeleza wajibu wao kikamilifu pindi alipowasili ofisini kwake na kuzungumza na watumishi wa ofisi yake waliompokea mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini. 

Mhe. Simbachawene amesema, rasilimaliwatu ni muhimu sana katika maendeleo ya taifa lolote, hivyo ni lazima ofisi yake ihakikishe watumishi wa umma wanafanya kazi kwa mujibu wa Kanuni, Sheria, Taratibu, Miongozo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo sheria mama ya nchi. 

Mhe. Simbachawene ameeleza kuwa, wateja wanaofuata huduma katika taasisi za umma wamekuwa wakilalamika kutopatiwa huduma nzuri na kwa wakati, na kuongeza kuwa, baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakifanya shughuli zao binafsi mahala pa kazi wakati wananchi wakisubiria kupatiwa huduma. 

“Muda ambao mtumishi wa umma anatakiwa kufanya kazi ni saa nane, lakini utakuta mtumishi akiingia kazini anakuwa na pilika nyingine ambazo si za kazi anayopaswa kuifanya, akitoa mfano wa Muuguzi au Mwalimu anaposhindwa kuwajibika, madhara yake ni makubwa na taifa linapata hasara kubwa kwasababu rasilimaliwatu haitumiki ipasavyo,” Mhe. Simbachawene amesisitiza. 

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, mtumishi anaingia kazini na simu ambayo ina makundi mengi, akianza kuwasiliana na makundi matatu tu saa moja ya kazi imeondoka na kwa kuwa ana makundi ya majirani, vikoba na mengineyo hivyo akiendelea kushiriki kinachojadiliwa unakuta matumizi ya simu yanachukua muda mwingi wa kazi na kusababisha wananchi kutopatiwa huduma wanayostahili. 

“Mimi niwaombe watumishi wenzangu na wataalam wangu tushirikiane na tuwe wazi ili tupate mwelekeo sahihi wa namna ya kurekebisha hii changamoto ya watumishi wa umma kutumia muda wa kazi vibaya badala ya kuwahudumia wananchi ambao kodi zao ndio zinatulipa mishahara,” Mhe. Simbachawene amesisitiza. 

Mhe. Simbachawene amefafanua kuwa, Serikali imewekeza rasilimalifedha kwa mtumishi wa umma ili aweze kutoa huduma kwa wananchi katika saa nane zote za kazi, hivyo ofisi yake inao wajibu wa kutafuta suluhisho la nini kifanyike kuhakikisha watumishi wa umma nchini wanatekeleza wajibu wao ipasavyo. 

Akitoa mfano wa nchi nyingine, Mhe. Simbachawene amesema kuwa watumishi hawaruhusiwi kutumia simu muda wa kazi ili waweze kutoa huduma iliyokusudiwa, na kuongeza kuwa waajiri wameweka utaratibu mzuri wa kuzihifadhi simu za watumishi pindi wanapoingia kazini na kuwapatia kwa ajili ya kuwasiliana na ndugu na jamaa zao wakati wa muda wa chakula cha mchana na wanapotoka kazini. 

Aidha, Mhe. Simbachawene amewashukuru watumishi wa ofisi yake kwa kumpokea vizuri na kuendelea kuomba ushirikiano wa kiutendaji ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza azma yake ya kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika kwa wananchi na kuwa na tija katika maendeleo ya taifa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa ofisi yake alipowasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete, Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi na Wa kwanza kushoto na Naibu Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Xavier Daudi.


Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya Waziri huyo kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya kuanza kazi rasmi baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini. 


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi wa ofisi yake alipowasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini. Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi na Wa kwanza kushoto na Naibu Katibu Mkuu-UTUMISHI Bw. Xavier Daudi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mtumishi Bi. Gladnessy Mwandry alipowasili Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuanza kazi, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na watumishi wa ofisi yake alipowasili Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba kuanza kazi, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na menejimenti ya ofisi yake alipowasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na menejimenti ya ofisi yake (hawapo pichani) alipowasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika mazungumzo na menejimenti ya ofisi yake alipowasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Aprili, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini.

 


 

No comments:

Post a Comment