Monday, February 17, 2020

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika akitoa maelezo ya awali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango huo jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwangalia Msanii wa Muziki, Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa TASAF Dkt. Moses Kusiluka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Marais Wastaafu wa Awamu ya Pili, Tatu na Nne wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakionyesha Mpango wa Utekelezaji wa TASAF baada ya Rais Magufuli kuzindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu na Mwenyekiti wa TASAF Dkt. Moses Kusiluka.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika wakiwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo.  

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Mhe. Kikwete ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na waliosimama ni Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Thursday, February 13, 2020

RAIS MAGUFULI KUZINDUA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YA TATU YA TASAF



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari leo alipokuwa akizungumza nao kuhusu uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) utakaofanyika siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere , Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu IKULU na Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Dkt. Moses Kusiluka na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao leo kuhusu uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) utakaofanyika siku ya Jumatatu tarehe 17 Februari, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere , Dar es Salaam. 

Saturday, February 8, 2020

MHE. MKUCHIKA AITAKA TIRA KUHAKIKISHA KAMPUNI BINAFSI ZA BIMA ZINAFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA NCHI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifungua mafunzo ya maadili kwa kamati ya Uongozi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo. Kushoto ni Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania Dkt. Mussa Juma.
Washiriki wa mafunzo ya maadili kwa kamati ya Uongozi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya maadili kwa kamati ya Uongozi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo. Kulia kwake ni Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, Dkt. Mussa Juma na Naibu Kamishna wa Bima, Bi. Khadija Issa Said (kushoto kwake).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiagana na Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, Dkt. Mussa Juma baada ya kufungua mafunzo ya maadili kwa kamati ya Uongozi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo.

Sunday, February 2, 2020

TAASISI ZA KIFEDHA ZAITHIBITISHIA SERIKALI KUTOA MIKOPO KUPITIA HATIMILIKI ZA KIMILA




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Inzomvu, Wilayani Mpwawa jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akitoa Hatimiliki ya Kimila kwa mmoja wa Wananchi wa Kijiji cha Inzomvu, Wilayani Mpwawa jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Kijiji cha Inzomvu Wilayani Mpwapwa aliowapatia Hatimiliki za Kimila jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA). Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na kushoto ni Mbunge wa Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje.

Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe akitoa taarifa ya utekelezaji wa MKURABITA katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) jana wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA) Wilayani Mpwapwa.

Mwakilishi wa Taasisi za Kifedha nchini ambaye ni Meneja wa NMB Tawi la Mpwapwa, Bi. Beatrice Mwasa akimthibitishia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) kuwa taasisi hizo ziko tayari kuwakopesha wananchi ili kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na wananchi kupitia hati hizo.

Baadhi ya wanufaika wa Hatimiliki za Kimila wa Kijiji cha Inzomvu Wilayani Mpwapwa wakiangalia Hati zao mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) jana wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA).

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Inzomvu Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao jana wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge  Tanzania (MKURABITA).