Thursday, May 16, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE AMEWATAKA WAHITIMU WA MAFUNZO YA UONGOZI KUWA MFANO BORA KWA JAMII

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amewataka Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi kuwa mfano katika jamii na kutumia taaluma waliyoipata kwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uwazi na haki.

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo tarehe 17 Mei,2024 katika Ukumbi wa Mliman City Jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya saba ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto EE cha Nchini Finland.

“Mafunzo ya uongozi yanathamani kubwa sana, hivyo, tunataka kuona uongozi wa kimkakati wenye manufaa zaidi katika usimamizi wa rasilimaliwatu na fedha, tunataka kuona mnaboresha nyanja ya mawasiliano na mahusiano baina yenu na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ndani na nje ya nchi” amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa Kiongozi mzuri ni yule anayewajibika na kuhakikisha anaacha alama, kwa mantiki hiyo hategemei kuona wahitimu hao wanakwenda kufanya kazi kwa mazoea bali watatumia uwezo wao na elimu waliyoipata kuleta matokeo chanya kwa ustawi kwa jamii.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Kikwete amewataka wahitimu hao kuwa chachu na kuleta mapinduzi katika maeneo yao ya kazi huku akiwasisitiza kuendelea kusoma zaidi kwa manufaa yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

“Kutokana na taarifa ya mafunzo mliyopata, mimi binafsi sitarajii kusikia wala kuona mnaendekeza tabia ya kutumia simu muda wa kazi wakati wananchi wanasubiri huduma na majibu ya changamoto zinazowakabili” alisema Mhe. Kikwete.

Aidha, Mhe. Kikwete ameto rai kwa wahitimu hao kutambua kuwa dhima kubwa ya uongozi ni kuonesha njia sahihi kwa wengine ili kuleta maendeleo ya haraka na yenye ufanisi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo kwa viongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam na kuzisaidia taasisi mbalimbali pamoja  na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu. 

Taasisi ya UONGOZI (UONGOZI INSTITUTE) ilianzishwa Julai, 2010 kwa malengo ya  kuwa na kituo cha utalaam wa juu cha kuendeleza viongozi Barani Afrika kwa kuanzia nchini Tanzania, Kanda za Afrika Mashariki na hatimaye Afrika nzima.

Katika Mahafali hayo ya saba ya Taasisi ya UONGOZI, jumla ya wahitimu 198 wamefuzu na kutunukiwa vyeti wakiwemo Watumishi wa Umma na Sekta binafsi katika Astashahada ya Uzamili katika Uongozi, Mafunzo ya Uongozi ngazi ya Cheti, na Mafunzo ya Uongozi kwa Wanawake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said akihimiza uwajibikaji kwa Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akielezea maudhui ya mafunzo yanayotolewa na taasisi yake wakati mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI ya wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti wakionesha vyeti walivyotunukiwa na Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya UONGOZI wakifuatilia mahafali ya saba ya Taasisi ya UONGOZI ya wahitimu wa Stashahada ya Uzamili ya Uongozi, Programu ya Uongozi kwa Wanawake na Programu ya Uongozi ngazi ya Cheti yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.







 


Thursday, May 9, 2024

SERIKALI KUBAINI MWENENDO WA UTENDAJI KAZI WA WATUMISHI WA UMMA

 Mwandishi Wetu

Tarehe 08 Mei, 2024

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi, amewataka Vinara wa  Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma PEPMIS kujitoa wakati wote kuwaelekeza watumishi wengine katika maeneo yao ya kazi ili Serikali iweze kubaini mwenendo halisi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Bw. Daudi, amesema hayo leo Mei 8, 2024 wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Vinara takribani 110 wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma kutoka katika taasisi mbalimbali za umma zilizopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Aidha, amewapongeza Vinara hao kwa kuchaguliwa na kupata fursa ya kujengewa uwezo ili kwenda kuwasaidia watumishi wengine katika taasisi mbalimbali zilizopo katika mikoa yao.

Pia, amewasisitiza Vinara hao kutambua kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewaamini na kuwapa dhamana kubwa ya kutoa msaada wa kiufundi kwa watumishi wengine katika masuala ya matumizi ya mfumo wa PEPMIS. Hivyo, wanatakiwa kutumia dhamana hiyo kwa ufanisi.

“Ninatambua mafunzo kama haya yalitolewa kwa watumishi wote katika kipindi cha mafunzo ya awali na ninyi mkiwa ni sehemu ya washiriki hao, sasa mumechaguliwa kuwa vinara kutokana na uwezo wenu, shauku na mapokeo chanya ya matumizi ya mifumo hii, hivyo jitoeni zaidi na muwe sehemu ya watumishi watakaotambuliwa na  Serikali na vizazi vijavyo kuwa sehemu ya waliofanya mageuzi katika utumishi wa umma” amesisitiza Bw. Daudi.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi, Ofisi ya Rais UTUMISHI Bi. Elizabeth Makyao amesema Mifumo ya PEPMIS na PIPMIS ni mipya na inahitaji wataalamu wengi ambao wanauwezo wa kutoa msaada wa kiufundi kwa ukaribu, haraka na ufanisi ili kuondoa changamoto ya kutafuta msaada huo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko tayari kupokea jambo ambalo litakuwa nje ya uwezo wao na kusaidia kupata ufumbuzi wa haraka kwa maendeleo ya taifa.

Aidha, mafunzo hayo ya siku tatu ni matokeo ya mapendekezo ya Timu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora walioshiriki kutoa na kusimamia mafunzo ya PIPMIS na PEPMIS kuanzia Novemba 23, 2023 hadi Februari 15, 2024 katika taasisi zote za umma zilizopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara.


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi akitoa hotuba wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Vinara wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma yanayofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi, Ofisi ya Rais UTUMISHI Bi. Elizabeth Makyao akizungumzaa jambo na Mgeni Rasmi Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Bw. Xavier Daudi kabla ya kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Vinara wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma yanayofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi, Ofisi ya Rais UTUMISHI Bi. Elizabeth Makyao akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Vinara wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma yanayofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.



Baadhi ya Vinara wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma (PIPMIS) kutoka katika taasisi mbalimbali za umma zilizopo katika mikoa 26 ya Tanzania Bara wakiwa kwenye mafunzo ya PEPMIS yanayofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma leo tarehe 8 Mei, 2024


Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Vinara wa Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma yanayofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


Monday, May 6, 2024

KATIBU MKUU KIONGOZI MHANDISI ZENA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUHESHIMIANA

 Na Mwandishi Wetu

Tarehe 06 Mei, 2024

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said amesisitiza Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania kuwaheshimu watumishi wote wa umma hata kama ni wa kada ya chini kwa kuwa kila mmoja anamchango wake kwa ustawi wa taasisi na Taifa kwa jumla.

Mhandisi Zena ametoa kauli hiyo leo Mei 6, 2024 wakati wa kufungua Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

“Tunahitaji kutoa heshima kwa kila mtu kwa kuwa kila binadamu anastahili heshma, iwapo tutawadharau wahudumu wetu kwa kuona kuwa ni kada ya chini tutajikuta tutakosa watu wa kutuhudumia, hivyo tutashindwa kufanya kazi zetu za msingi”ameongeza Mhandisi Zena.

Aidha, Mhandisi Zena amewakumbusha Mameneja hao kutambua kuwa, vyeo vya watumishi wa umma kwa kada zote ni muhimu sana na viliwekwa kwa sababu maalum. Kwa mantiki hiyo, kila mtumishi kwa nafasi yake anatakiwa kuheshimiwa kwa kuwa anamchango katika kuhakikisha dira ya taifa inafikiwa kwa haraka na kwa ufanisi.

Vilevile, amewataka Mameneja hao kuwa wazalendo, kutamani kuona maendeleo ya Taifa, kutotaja majina ya viongozi wakuu bila sababu ya msingi kuwa wamepewa maelekezo kutoka juu, kuacha tabia ya kubeza kwa namna yoyote ile siku na sherehe za kitaifa, isipokuwa wanatakiwa kuziheshimu na kuzienzi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Awali, Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu Barani Afrika ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi, amesema kuwa mtandao huo unatumika kama njia ya kuweka pamoja Mameneja Rasilimaliwatu Barani Afrika na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuboresha utendaji kazi katika nchi zao kwa lengo la kuleta maendeleo ya haraka.

“Sasa hivi tunashuhudia matumizi makubwa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano -TEHAMA katika utendaji kazi, hivyo uwepo na ukuaji huu wa teknolojia mathalani matumizi ya Akili Bandia (Artificial Intelligence-AI) hatuna budi kama Bara la Afrika kuongeza jitihada za ukuaji wa Mtandao huu ili nchi zote Barani Afrika ziweze kutumia teknolojia hizi kwa maendeleo” amebainisha Bw. Daudi.

Aidha, ameongeza kuwa Mtandao utasaidia Bara la Afrika kuwa na wataalamu wa rasilimaliwatu wenye sifa na ubora ili waweze kuzisaidia nchi zao kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo.

Pia, Bw. Daudi ametumia fursa ya mkutano huo kuhamasisha watu kushiriki kwa wingi kwenye mkutano wa mwaka wa Bara la Afrika ambao utafanyika mwezi Novemba, 2024 nchini Tanzania. Mkutano huo utatumika kubadilisha uzoefu na zaidi kukuza na kuongeza uchumi wa Taifa.

Mkutano huo ulifanyika kwa siku moja umetumika kuzindua rasmi Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania (TPS-HRMnet).

Mhe. Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa akiwa na Viongozi mbalimbali kabla ya kumpokea Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Eng. Zena Ahmed Said kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania-TPS HRMnet katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)AICC leo tarehe 6 Mei, 2024.


Mhe. Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa akimpokea Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Eng. Zena Ahmed Said katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania-TPS HRMnet leo tarehe 6 Mei, 2024.


Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Eng. Zena Ahmed Said akiteta jambo na Mhe. Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakati wa kufungua Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania leo tarehe 6 Mei, 2024.


Mhe. Xavier Daudi, Rais wa APS HRMnet-Africa ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora akitoa salaamu za APSHRMnet -Afrika kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania leo tarehe 6 Mei, 2024.


Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Eng. Zena Ahmed Said akihutubia washiriki wa Mkutano wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Barani Afrika, Tawi la Tanzania unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) leo tarehe 6 Mei, 2024.





Saturday, May 4, 2024

NAIBU WAZIRI KIKWETE ASISITIZA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA ILI KUIMARISHA HAKI NA WAJIBU

 Na Mwandishi Wetu

Tarehe 04 Mei, 2024

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Maafisa Utumishi kutumia mifumo ya usimamizi wa rasilimaliwatu iliyosanifiwa na kutengenezwa na Serikali kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi na kuleta uwazi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo leo Mei 4, 2024 wakati akifunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Amesema kuwa, Serikali imetengeneza mifumo mbalimbali akitolea mfano wa Mfumo wa Employment Self Service (ESS) ambao moja ya lengo lake ni kuwawezesha watumishi wa umma kupata huduma kwa urahisi na kupunguza mlolongo na ukiritimba uliokuwepo katika taratibu za kupata huduma za mikopo katika taasisi za umma na taasisi za fedha. 

“Serikali imelenga kutengeneza mazingira rafiki na kuwafanya watumishi wa umma kutumia muda wa kazi katika kuwahudumia wananchi kwa haraka na wakati, hivyo, waelimisheni watumishi walio katika sehemu zenu za kazi ili kutumia mifumo hiyo kwa ufanisi” amesisitiza Mhe. Kikwete.

Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetafsiri kwa ufanisi na kutekeleza azma na maagizo ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa na nia ya kuifanya Serikali kuwa ya kidijitali kwa kuandaa mifumo inayorahisisha utendaji kazi.

“Rais wetu amelenga kubadilisha mfumo wa utumishi wa umma ili uendane na Tanzania anayoitaka, hivyo, sisi tukiwa ndio wasaidizi wake na watumishi wa umma kwa jumla hatuna budi kuhakikisha azma yake inatekelezwa ipasavyo kwa kutumia mifumo hiyo” ameongeza Mhe. Kikwete. 

Mhe. Kikwete ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimawatu kuhakikisha wanasimamia mifumo hiyo ya Serikali na kuwahimiza watumishi katika taasisi zao kuitumia kwa lengo lililokusudiwa na Serikali.

“Iwapo kutatokea kushindwa kutumika ipasavyo itakuwa ni sehemu ya kushindwa katika uongozi wenu na shughulikieni kero za wananchi ili Tanzania anayoitaka Rais, Mhe. Samia iweze kupatikana” ameongeza Mhe. Kikwete.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Kikwete kufunga mkutano huo, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi amesema washiriki wa mkutano huo wamepata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali yatakayoboresha utendaji kazi na kuongeza tija na ufanisi.

Mkutano huo wa siku tatu unaoratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, umehitishwa leo kwa kufanya uchaguzi na kuwapata viongozi wa Jumuiya ya Maafisa Tawala na RasilimawatuTanzania (TAPAHR)

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa hatuba ya kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi yake Bw. Xavier Daudi kabla ya kutoa hatuba ya kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Mwenyekiti wa AAAPM Tawi la Tanzania, Bi. Leila Mavika akitoa maelezo mafupi kuhusu AAPAM Tawi la Tanzania kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kabla ya kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Rais wa AAPAM Afrika, Dkt. John Nakabago akitoa kitambulisho cha uanachama wa AAPAMA Tawi la Tanzania kwa Makamu wa Rais wa AAPAM, ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Ayoub J. Kilabuka wakati wa kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo wakati wa akitoa hatuba ya kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania wakifuatilia wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa neno la utangulizi wakati wa kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).



Friday, May 3, 2024

MAELEKEZO YA MHE. WAZIRI SIMBACHAWENE KWA WAKUU WA IDARA ZA UTAWALA NA RASILIMALIWATU


 

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WATUMISHI WENYE DHAMANA YA KUINGA KWENYE MIFUMO YA KIUTUMISHI KUTENDA HAKI

 Na. Rainer Budodi-Arusha

Tarehe 02 Mei, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Maafisa Utumishi waliopewa dhamana ya kuingia kwenye mifumo ya usimamizi wa rasilimaliwatu kutumia dhamana hiyo kutochezea mifumo hiyo na kuwaonea watumishi wengine na badala yake watumie dhamana hiyo kutenda haki.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Amesema kuwa yapo malalamiko yanayoonesha uvunjifu wa Maadili na ukiukwaji wa taratibu za kiutendaji ikiwemo, baadhi ya Maafisa Utumishi ambao wanaingia katika Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (New HCMIS) kusimamisha mishahara au makato ya mishahara bila kufuata taratibu zilizowekwa na wakati mwingine kutumia nafasi zao kukomoa watumishi wengine, lakini pia wamekuwa wakitoa taarifa ambazo wanakutana nazo katika mifumo hiyo kwa watu wasiohusika.

“Tumebaini baadhi mnafanya hivyo kwa sababu tu mna dhamana ya kuingia kwenye mifumo, hili limejitokeza sana, tufahamu kuwa Sheria zetu za TEHAMA na za kiutumishi zinatambua kuwa hayo ni makosa makubwa ya Kimenejimenti na sehemu kubwa ni makosa ya jinai, hivyo tutachukua hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kufanya hivyo,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Mhe. Simbachawene ametumia fursa kutoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya kusimamia mifumo hiyo ya serikali ili isichezewe kwani imekuwa msaada mkubwa katika kuboresha ufanisi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma nchini.

“Wenzetu Viongozi mlioko kwenye mikoa na Wilaya mtusaidie kusimamia hili  kwani masuala ya utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu ni ya wote na sio ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora pekee,  hivyo tukiruhusu mifumo hii kuchezewa tutashindwa kufikia malengo ya serikali ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi,  tushirikiane kuwabaini wale wanaoihujumu ili hatua kali zichukuliwe kwa masilahi mapana ya taifa,” Mhe. Simbachawene ameongeza.

Ameongeza kuwa mifumo hiyo imeisaidia Serikali kudhibiti baadhi ya mambo ya hovyo ambayo yamekuwa yakifanywa na baadhi ya watu, hivyo wale wote wanaopenda mambo ya hovyo wanaihujumu ili isifanye kazi na kurudisha nyumba maendeleo ya nchi.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Simbachawene kufungua mkutano huo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rai-UTUMISHI, Bi. Felister Shuli amesema mkutano huo wa 11 umelenga kutoa fursa kwa wataalam na wasimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala katika Utumishi wa Umma kujifunza; kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu; na kubaini changamoto zinazojitokeza katika kusimamia rasilimaliwatu na namna ya kukabiliana nazo.  

Aidha, umelenga kuweka mikakati ya kuendeleza Utawala na Rasilimaliwatu kwa kuzingatia makubaliano ambayo yamefikiwa na nchi wanachama wa AAPAM Afrika ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Serikali kwa umma.

Mkutano huo wa siku tatu unaoratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora-Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu unaongozwa na Kaulimbi isemayo ‘Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utoaji wa Huduma: Nafasi ya TEHAMA katika kuimarisha Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma.’

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifungua Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).



Rais wa AAPAM Afrika, Dkt. John Nakabago akitoa salam wakati wa Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Mwenyekiti wa AAAPM Tawi la Tanzania, Bi. Leila Mavika akitoa utambulisho na maelezo kuhusu AAPAM Tawi la Tanzania kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri huyo kufungua Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Felister Shuli akitoa maelezo ya awali kuhusu Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kufungua Mkutano huo leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Washiriki wa Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).