Tuesday, May 28, 2019

VIONGOZI NA WATUMISHI WA WIZARA YA MADINI WATAKIWA KUWA WAADILIFU KATIKA UTENDAJI KAZI WAO ILI TANZANIA IWEZE KUFIKIA UCHUMI WA KATI IFIKAPO MWAKA 2025


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifungua mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi cheti cha ufanyakazi bora kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa Wizara ya Madini, Bi. Asteria Muhozya baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (Mb) (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini  Bw. Issa Nchasi (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) na Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (Mb) wakifurahia jambo baada ya ufunguzi mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini  Bw. Issa Nchasi.

Wednesday, May 22, 2019

NAIBU KATIBU MKUU-UTUMISHI AFUNGA SEMINA YA KUZIJENGEA UWEZO NCHI WANACHAMA WA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA KUHUSU UTEKELEZAJI NA UTOAJI WA TAARIFA ZA MKATABA WA MISINGI NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BARANI AFRIKA



Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akifunga Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji na utoaji wa tarifa za Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala Barani Afrika iliyomalizika leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akimsikiliza Mwakilishi wa Kurugenzi inayoshughulikia Masuala ya Siasa Umoja wa Afrika, Bw. Issaka Garba Abdou wakati wa kufunga Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji na utoaji wa tarifa za Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala Barani Afrika iliyomalizika leo jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wajumbe wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji na utoaji wa tarifa za Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala Barani Afrika wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael alipokuwa akifunga semina hiyo jijini Dar es Salaam.

Monday, May 20, 2019

DKT. MWANJELWA AFUNGUA SEMINA YA KUZIJENGEA UWEZO NCHI WANACHAMA WA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MISINGI NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA NA UTOAJI WA TAARIFA BARANI AFRIKA



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifuatilia maelezo ya Mwakilishi wa Kurugenzi inayoshughulikia Masuala ya Siasa Umoja wa Afrika, Bw. Issaka Garba Abdou wakati wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokuwa akifungua semina hiyo jijini Dar es Salaam.

Mjumbe kutoka Tanzania, Bwana Gubas Vyagusa akizungumza kwenye Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.