Wednesday, December 20, 2017

TUNATEKELEZA 2018, USIKOSE

TUNATEKELEZA-FUNGUA MWAKA 2018, USIKOSE!

TUNATEKELEZA-FUNGUA MWAKA 2018, USIKOSE! KUJUA MASUALA MBALIMBALI YA KIUTUMISHI NCHINI TANZANIA.


Sunday, December 10, 2017

MAADILI NI SUALA LETU SOTE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa Disemba 10, 2017 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu.) Mhe. George Mkuchika (Mb) akizungumza kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzungumza na wananchi.

Baadhi ya watumishi na wananchi waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa Disemba 10, 2017 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika meza kuu na baadhi ya viongozi wa Serikali katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa Disemba 10, 2017 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika banda la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akipokea maelezo ya kiutendaji ya ofisi hiyo.

Mwanasheria  Mkuu wa Serikali  Bw. George Masaju (kulia) akisisitiza jambo kwa maofisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, alipolitembelea banda la ofisi hiyo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.