Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifuatilia maelezo kuhusu Tovuti ya Watumishi
(Watumishi Portal) baada ya kuizindua rasmi mkoani Dodoma leo. Kulia kwake ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) na kushoto kwake ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura
(Mb) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro.
|