Sunday, September 27, 2015

MAPOKEZI YA MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS-UTUMISHI MHE. CELINA O. KOMBANI (MB)

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (Mb) ukipokelewa katika Kiwanja cha ndege cha Mwalimu J.K Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka nchini India jana jioni.

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa na waombolezaji wengine wakisubiri kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi katika Kiwanja cha Mwalimu J.K Nyerere jana jioni.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Add caption

Pumzika kwa Amani mpendwa wetu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (pichani).
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na watumishi wote wa Ofisi ya Rais-Utumishi wataendelea kukukumbuka daima kwa busara zako na uongozi wako mzuri.
                                                                                                   

Wednesday, September 23, 2015

Marehemu Yakalawa Kondo enzi za uhai wake

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Yakalawa Kondo – Msaidizi wa Ofisi Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Pichani) kilichotokea tarehe 21.09.2015 saa 3 usiku katika Kituo cha Afya cha Vijibweni - Kigamboni. Mazishi yalifanyika tarehe 22.09.2015 saa 10 jioni katika makaburi ya Tungi Shule – Kigamboni.

“Mungu ailaze  Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amen”


Tuesday, September 15, 2015

UTUMISHI YAFANYA KIKAO KAZI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (VIDEO CONFERENCE)

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifungua kikao kazi kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference)kilichojumuisha Ofisi ya Rais-Utumishi na Mikoa ya Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Lindi, Dodoma, Geita, pamoja na Ofisi za Wizara ya Fedha, TAMISEMI, Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Tume ya Utumishi wa Umma na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (kushoto) wakifuatilia mada zinazowasilishwa wakati wa kikao kazi kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference)kilichojumuisha Ofisi ya Rais-Utumishi na Mikoa ya Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Lindi, Dodoma, Geita, pamoja na Ofisi za Wizara ya Fedha, TAMISEMI, Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Tume ya Utumishi wa Umma na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.  

Monday, September 14, 2015

BONANZA LA WATUMISHI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI LAFANA VIWANJA VYA LEADERS CLUB

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa tatu kutoka kulia) akifanya mazoezi  na Watumishi wa ofisi yake wakati wa Bonanza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika Leaders Club siku ya Jumamosi Septemba 12, 2015.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakifanya mazoezi ya viungo wakati wa Bonanza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika Leaders Club siku ya Jumamosi Septemba 12, 2015.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akifungua Bonanza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika katika Viwanja vya Leaders Club siku ya Jumamosi Septemba 12, 2015.

Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakishindana kukimbia na gunia wakati wa Bonanza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika Leaders Club siku ya Jumamosi Septemba 12, 2015.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa mbio za magunia Bw. Ally Litongolele (kulia) wakati wa Bonanza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika Leaders Club siku ya Jumamosi Septemba 12, 2015.

Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakishindana kukimbia na yai wakati wa Bonanza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika Leaders Club siku ya Jumamosi Septemba 12, 2015.