Thursday, August 27, 2015

WATUMISHI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAPATA MAFUNZO KUHUSU VVU NA UKIMWI NA NAMNA YA KUISHI KWA MTINDO BORA WA MAISHA

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa kwanza kutoka kulia) na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo wakifuatilia mada kuhusu VVU na UKIMWI na namna ya kuishi kwa mtindo bora wa maisha katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Utumishi mapema jana.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akiwasisitiza watumishi wa Ofisi hiyo kuzingatia mafunzo waliyoyapata kuhusu VVU na UKIMWI na namna ya kuishi kwa mtindo bora wa maisha katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Utumishi mapema jana. Kushoto kwake ni Dkt. Hafidh Ameir kutoka TACAIDS.

Mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (kulia) akipima VVU na UKIMWI baada ya kupata mafunzo kuhusu VVU na UKIMWI na namna ya kuishi kwa mtindo bora wa maisha katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Utumishi mapema jana.

Wednesday, August 19, 2015

Mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao wafunguliwa rasmi jijini Arusha

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akifungua mkutano wa kwanza wa Serikali Mtandao kwa Watendaji Wakuu na Viongozi wa Serikali, Arusha.

Sehemu ya washiriki wa mkutano wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue (hayupo pichani).

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akikaribishwa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu katika mkutano kuhusu Serikali Mtandao katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Thursday, August 13, 2015

Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi lafanyika

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu akifungua mkutano wa  baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa  Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Dar es Salaam.

Watanzania walionufaika na ufadhili wa masomo nchini Japan Waagwa

Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Watanzania walionufaika na ufadhili wa masomo wa mpango wa ABE Initiative unaoratibiwa na JICA.  
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa sita kutoka kulia) na Balozi wa Japan nchini Bw. Masaharu Yoshida (wa tano kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watanzania wakionufaika na ufadhili wa mpango wa ABE baada ya hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani. Wengine ni Maofisa kutoka Utumishi na JICA.

Mkutano wa masuala Serikali Mtandao kufanyika jijini Arusha

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mkutano wa Serikali Mtandao utakaowakutanisha Watendaji Wakuu na Maofisa wa Ngazi na Fani Mbalimbali kutoka Serikalini utakaofanyika jijini Arusha Agosti 17-20,2015. 

Wednesday, August 12, 2015

Mwili wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Boniphace O. Haule aliyefariki nchini India,wawasili jijini Dar es Salaam

Mwili wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Boniphace O. Haule ukiwa katika gari baada ya kupokelewa katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu J.K Nyerere.


Tuesday, August 11, 2015

TANZIA



Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Boniphace Haule - Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Pichani) kilichotokea nchini India tarehe 10.08.2015.
Mwili wa Marehemu utawasili leo, uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere. Mazishi yatafanyika Ijumaa tarehe 14/08/2015. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tegeta Ununio, Mtaa wa Mwaitende.

Maziko yanatarajia kufanyika katika makaburi ya KINONDONI.

Taarifa na taratibu za msiba zitafuata.

Monday, August 10, 2015

Taswira wakati wa Uzinduzi wa Kantini ya Kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo

Keki rasmi iliyotumika wakati wa uzinduzi wa kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu akikata utepe kuzindua rasmi kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma baada ya ukarabati.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu akimlisha keki Mmiliki wa Kampuni ya Runners Catering  inayotoa Huduma ya Chakula Bi.Nuru Nassib mara baada ya kuzindua rasmi kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu akimlisha keki Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, Utumishi Bw. Aloyce Msigwa mara baada ya kuzindua kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi mapema leo.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu akilishwa keki na Mmiliki wa Kampuni ya Runners Catering  inayotoa Huduma ya Chakula Bi.Nuru Nassib mara baada ya kuzindua rasmi kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo.
 Wahudumu wa Kampuni ya Runners Catering  inayotoa Huduma ya Chakula  wakiendelea kutoa huduma mara baada ya uzinduzi wa kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu (katikati) akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais - Utumishi na Mmiliki wa Kampuni ya Runners Catering  inayotoa Huduma ya Chakula Bi.Nuru Nassib (kulia) wakati wa uzinduzi wa  kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Utumishi wakipewa huduma na wahudumu wa Kampuni ya Runners Catering  inayotoa Huduma ya Chakula baada ya kuzindua rasmi kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mapema leo.
Taswira ya moja ya sehemu ya kantini ya kisasa ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Friday, August 7, 2015

UTUMISHI YAKABIDHIWA ZAWADI YA USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA YALIYOFANYIKA CONGO BRAZAVILLE

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akipokea cheti cha ushiriki wa Tanzania kutoka kwa Mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma  Barani Afrika yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni.  
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akionyesha cheti cha ushiriki wa Tanzania katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni.  Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji kutoka ofisi ya Rais-Utumishi na mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo kutoka Wizara ya Uchukuzi Bw. William Budoya (kulia).

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akipokea zawadi ya Tanzania kutoka kwa mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni.