James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam
Tarehe 23 Februari, 2021
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewahiza
Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kuendelea kufanya kazi kwa
bidii ili kuboresha huduma zitolewazo na Wakala hiyo.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo leo wakati
wa ziara yake ya kikazi katika Wakala hiyo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la
kujitambulisha, kufahamu kwa kina makujumu ya Wakala hiyo, kuzitafutia ufumbuzi
changamoto zinazowakabili watumishi wa Wakala hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
Mhe. Ndejembi amewapongeza
Watumishi wa Wakala hiyo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na weledi
kwani hakuna maafa yoyote yaliyowahi kujitokeza tangu Serikali ianze kumiliki
ndege zake.
Mhe. Ndejembi amesema, Wakala hiyo
ina jukumu kubwa la kuhakikisha matengenezo ya ndege yanafanyika kwa wakati ili
ziendelee kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa Mhe. Rais na Viongozi Wakuu wa
Serikali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za Viongozi hao wa Kitaifa
zinatekelezwa kama zilivyopangwa.
Aidha, Mhe. Ndejembi ameahidi
kuzifanyia kazi changamoto za Wakala hiyo ili kuwawezesha Watumishi wa Wakala
hiyo kuwa na mazingira bora yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao
kikamilifu.
Mhe. Ndejembi amewaasa watumishi
hao kuendelea kuchapa kazi wakati changamoto zao zikifanyiwa kazi.
Wakala ya Ndege za Serikali
ilianzishwa tarehe 17 Mei, 2002 kwa mujibu wa Sheria ya Wakala ya Ndege za
Serikali Na.3 ya Mwaka 1997 kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha usalama
wa usafiri wa ndege kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wanaotumia ndege hizo. Pamoja
na jukumu hilo, Wakala ina jukumu la kuratibu kwa niaba ya Serikali ununuzi wa
ndege mpya za biashara, kuzikodisha kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na
kusimamia mikataba ya ukodishwaji wa ndege hizo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na
Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) alipofanya ziara ya kikazi
katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Watumishi wa Wakala ya Ndege za
Serikali (TGFA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya
kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji.
Mtumishi wa Wakala ya Ndege za
Serikali (TGFA), Salahe Harun Mwanauta ambaye ni Rubani akiwasilisha hoja kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini
Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mtumishi wa Wakala ya Ndege za
Serikali (TGFA), Bernard Joseph Mayila akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam
yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
akizungumza na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) alipofanya
ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la
kuhimiza uwajibikaji.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Ndege za Serikali (TGFA) Dkt. Benjamin Ndimila akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa majukumu ya Wakala yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji.