Thursday, May 28, 2020

DKT. MWANJELWA AIPONGEZA TPSC KUUNDA VIKOSI KAZI DHIDI YA CORONA ILI KUTEKELEZA AGIZO LA KUPOKEA WANAFUNZI JUNI MOSI, 2020



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)  akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Kampasi ya Singida (hawapo pichani)  mara baada ya kupokea taarifa ya Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo hicho kuhusu Mkakati wa Uendeshaji Mafunzo kwa Kuzingatia Tahadhari Dhidi ya Maambukizi ya Corona, utakaoanza kutekelezwa na Chuo hicho pindi kitakapofunguliwa tarehe 01/06/2020.

Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Singida wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (hayupo pichani) mara baada ya Naibu Waziri huyo kupokea taarifa ya Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo hicho kuhusu Mkakati wa Uendeshaji Mafunzo kwa Kuzingatia Tahadhari Dhidi ya Maambukizi ya Corona.


Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika akimshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa kukitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma ili kujiridhisha na mkakati wa Chuo hicho katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona (COVID 19), kabla ya chuo hicho kufunguliwa tarehe 01/06/2020.


Fundi Bomba aliyepewa jukumu la kutengeneza mabomba ya maji tiririka nje ya geti la Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Singida ili kuwawezesha wafanyakazi, wanafunzi na wadau wa chuo kunawa mikono yao na sabuni kwa maji tiririka.


Tuesday, May 19, 2020

MKUCHIKA AZINDUA BODI YA USHAURI YA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI NA KUITAKA IHAKIKISHE ATCL INAKUWA IMARA KIUSHINDANI


MKUCHIKA AZINDUA BODI YA USHAURI YA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI NA KUITAKA IHAKIKISHE ATCL INAKUWA IMARA KIUSHINDANI





Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakala ya Ndege za Serikali (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi ambaye pia ni Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Ndege za Serikali akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kuzindua rasmi bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi ambaye pia ni Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Ndege za Serikali wakati akitoa neno la utangulizi kabla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Wakala ya Ndege za Serikali uliofanyika mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.




Wednesday, May 13, 2020

WAJUMBE BARAZA JIPYA LA MAADILI YA VIONGOZI WATAKIWA KUTEKELEZA WAJIBU WAO KWA WELEDI



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe.George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu, Mhe. Harold Nsekela alipokuwa akiwatambulisha Wajumbe wapya wa Baraza la Maadili ya Viongozi waliofika ofisini kwa Mhe. Waziri jijini Dodoma kujitambulisha. 



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe.George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Maadili ya Viongozi waliofika ofisini kwake jijini Dodoma kujitambulisha. Wa kwanza kulia kwa Mhe. Waziri ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na wa kwanza kushoto ni Mwenyeki wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Ibrahim Mipawa.