Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Kampasi ya Singida (hawapo pichani) mara baada ya kupokea taarifa ya Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo hicho kuhusu Mkakati wa Uendeshaji Mafunzo kwa Kuzingatia Tahadhari Dhidi ya Maambukizi ya Corona, utakaoanza kutekelezwa na Chuo hicho pindi kitakapofunguliwa tarehe 01/06/2020.
Baadhi ya watumishi wa Chuo
cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Singida wakimsikiliza Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (hayupo pichani) mara baada ya Naibu Waziri huyo kupokea
taarifa ya Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo hicho kuhusu Mkakati wa Uendeshaji
Mafunzo kwa Kuzingatia Tahadhari Dhidi ya Maambukizi ya Corona.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa
Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika akimshukuru
Dkt. Mwanjelwa kwa kukitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma ili kujiridhisha na
mkakati wa Chuo hicho katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona
(COVID 19), kabla ya chuo hicho kufunguliwa tarehe 01/06/2020.
Fundi Bomba aliyepewa jukumu
la kutengeneza mabomba ya maji tiririka nje ya geti la Chuo cha Utumishi wa
Umma Kampasi ya Singida ili kuwawezesha wafanyakazi, wanafunzi na wadau wa chuo
kunawa mikono yao na sabuni kwa maji tiririka.
No comments:
Post a Comment