Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph
akiwasisitiza Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha ujenzi
wa ofisi kwa wakati katika Mji wa Serikali ili iweze kutumika kuwahudumia
wananchi.
Afisa Ugavi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bw. Deograsius Michael (kulia) akikabidhi hati ya makabidhiano ya
kiwanja kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, Mhandisi
David H. Shunu (kushoto) kwa lengo la kuanza ujenzi wa Ofisi katika Mji wa
Serikali. Anayeshuhudia ni Afisa Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Bw. Benard Makanda.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph (wa
pili kushoto) akizungumza na Wataalamwa
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kukabidhi kiwanja kwa ajili ya
ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugezi wa Huduma za Ushauri wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
Dodoma, akiahidi kutimiza jukumu lake ili kuhakikisha ujenzi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora unakamilika kwa wakati katika
Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale akisisitiza jambo kwa TBA
ili kuhakikisha ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma
unakamilika kwa wakati.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akisaini Mkataba na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius
Mwakalingawa kuanza rasmi ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalingawakipeana mikono kabla ya kukabidhiana Mkataba wa kuanza rasmi ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbarona Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius
Mwakalinga wakionyeshaMkataba wa kuanza rasmi ujenzi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa
jijini Dodoma.