Monday, March 19, 2018

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA TAASISI ZAKE KWA KUTEKELEZA VIZURI MAJUKUMU KATIKA MWAKA WA FEDHA 2017/18

Add caption

Add caption

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akifungua kikao cha kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI  iliyowasilishwa kwenye kamati  hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Selasini (Mb) akichangia hoja kuhusu Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI  iliyowasilishwa kwenye kamati  hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa.

Sunday, March 18, 2018

KAMATI YA BUNGE YAKIPONGEZA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KWA UTENDAJI MZURI NA UJENZI WA JENGO KATIKA KAMPASI YA TABORA



Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Henry Mambo akitoa taarifa ya utekelezaji ya majukumu ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipokitembelea chuo hicho kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la chuo Kampasi ya Tabora.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Henry Mambo (kushoto) kwenda kushuhudia jengo la chuo Tawi la Tabora lililojengwa kwa jitihada za chuo kwa kutumia fedha za ndani.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jason Rweikiza (Mb) kushuhudia jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tabora (linaloonekana) lililojengwa kupitia mapato ya ndani ya chuo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa jengo la chuo Tawi Tabora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea Kampasi hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kampasi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akitoa pongezi kwa Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kwa ujenzi wa jengo la chuo katika Kampasi ya Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akiishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa kukitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la chuo katika Kampasi ya Tabora.