Friday, January 16, 2015

Utumishi yasaini mikataba Saba ya Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali (GOVNET), Awamu ya Pili



Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (kulia)akiwakabidhi mkataba wawakilishi wa kampuni zilizoshinda zabuni.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dr. Jabiri Kuwe Bakari (kulia)akikabidhiwa mkataba na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi katika kikao.
Baadhi ya washiriki  wa kikao hicho wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi  akitoa maelekezo kuhusu lengo la serikali kuleta huduma bora kwa Wananchi kupitia mtandao wa Mawasiliano wa Serikali (GOVNET).

Tuesday, January 13, 2015

MABADILIKO KATIKA KLABU YA MICHEZO YA UTUMISHI

Kamati iliyosimamia zoezi la uchaguzi wa viongozi wa klabu ya michezo ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Mwenyekiti Mpya wa Klabu ya Michezo ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Seushi Mburi akizungumza baada ya kuchaguliwa kuiongoza klabu hiyo katika uchaguzi ulichofanyika Utumishi hivi karibuni.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Tumishi wa Umma  Bi.Jane Kajiru akizungumza kuhusu umuhimu wa michezo mahala pa kazi.
Sehemu ya wagombea waliojitosa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi.
Sehemu ya wapiga kura waliojitokeza.
Sehemu ya wagombea waliojitosa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi.

Thursday, January 8, 2015

UTUMISHI YAITISHA KIKAO CHA WAKURUGENZI WA HUDUMA NA UENDESHAJI WA WAKALA ZA SERIKALI

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kulia) akizungumza katika kikao cha Wakurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa Wakala za Serikali kilichofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo. 
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Utumishi na washiriki kutoka Wakala za Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (hayupo pichani) katika kikao cha Wakurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa Wakala kilichofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Washiriki kutoka wakala mbalimbali za Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (hayupo pichani) katika kikao cha Wakurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa Wakala kilichofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi- Utumishi Bw. Nolasco Kipanda akizungumza wakati wa kikao cha Wakurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa Wakala kilichofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.