Wednesday, January 17, 2024

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA IKIPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA BUNGE

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao cha kamati yake, Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kilichofanyika katika ofisi za Bunge jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha kamati hiyo na Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watendaji wa taasisi za Wakala ya Ndege za Serikali, Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizo chini ya ofisi hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la utangulizi katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma kabla ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kilichofanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka akifafanua jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa Wakala ya Ndege za Serikali, Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Mashimba Ndaki akichangia hoja wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Viongozi na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa maelekezo na ushauri uliotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati ilipofanya ziara katika ofisi hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Eng. Benedict Ndomba akifafanua kuhusu utendaji wa mifumo ya TEHAMA Serikalini wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika katika ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Innocent Bomani akifafanua hoja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu mifumo ya ajira portal wakati wa kikao cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika katika ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wakala ya Ndege za Serikali, Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakiwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika katika ofisi za Bunge jijini Dodoma.


Maafisa wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wakala ya Ndege za Serikali, Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kamati na ofisi hiyo kilichofanyika katika ofisi za Bunge jijini Dodoma

 


 

Tuesday, January 9, 2024

MHE. SIMBACHAWENE AWAKUMBUKA WALIMU NA MANESI, AITAKA TAASISI YA WATUMISHI HOUSING INVESTMENT KUWAJENGEA MAKAZI BORA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameitaka  Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) kuja na ubunifu wa kujenga makazi bora ya watumishi wa umma katika maeneo ya mijini  jirani na maeneo ya shule na hospitali  ili kuwaondolea changamoto ya makazi manesi na walimu  kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao 

Amesema maeneo ya mijini, shule pamoja na hospitali zinamiliki maeneo makubwa ambayo Taasisi ya WHI inaweza kuyatumia kujenga majengo marefu kwenda juu ili kuwafanya walimu na  manesi wafurahie kutoa huduma kwa wananchi kwa kuishi kwenye makazi bora jirani na maeneo ya kazi 

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Timu ya Menejimenti ya Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) ikiwa ni muendelezo wa kusikiliza changamoto zinazoikabili Taasisi anazozisimamia  pamoja na kufuatilia  utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara aliyoifanya Mwezi Agosti mwaka jana

Amesema katika maeneo ya mijini watumishi wakiwemo walimu na manesi wamekuwa wakilazimika kutafuta makazi  mbali na maeneo wanakofanyia kazi kwa vile ni vigumu kupata nyumba karibu na maeneo hayo na hata makazi yakipatikana  gharama zake za kulipia huwa ni kubwa kulingana na kipato chao.

'' Hakuna asiyejua umuhimu wa walimu na manesi katika nchi hii lakini lakini wengi wa wamekuwa wakiishi maeneo ya mbali na wanakofanyia kazi na hivyo kulazimika kulipa nauli kubwa kwa vile hawawezi kumudu kulipa kodi ya makazi yaliyo jirani na maeneo yao ya kazi, waguseni hawa kwa kuwajengea makazi bora. amesema Mhe. Simbachawene

Mhe.Simbachawene amesisitiza kuwa Nyumba zikiwa jirani na eneo la kazi inasaidia kupunguza gharama za maisha na kuongeza ufanisi kazini na hilo ndio lengo haswa la Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha watumishi wanafurahia mazingira ya kazi kwa gharama rafiki"

Amesema Watumishi wa Umma wakiwemo walimu na manesi wanaofanya kazi katika maeneo ya mijini wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kutokana na changamoto ya makazi na hivyo kupelekea kutoa huduma zisizoridhisha kwa wateja wao.

Mhe. Simbachawene amesema kitendo cha watumishi wa umma kutokuwa na makazi bora na kuwa mbali na maeneo yao wanayofanyia kazi ni changamoto kubwa inayoathiri utendaji kazi, hivyo ameitaka  taasisi hiyo kuona umuhimu wa kufanya hivyo kwani utekelezaji wq ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/ 2025  

Mhe. Simbachawene amesema ujenzi wa  makazi bora hayo  karibu na maeneo ya kazi, kutawasaidia watumishi  wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza maeneo  kutohangaika. “Mkijenga nyumba maeneo ya jirani na vituo vya kazi, kutawasaidia sana watumishi kutoichukia kazi kwa watapata sehemu nzuri ya kuishi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.


Kwa upande wake Mkurugezi wa  Taasisi ya  Watumishi Housing, Dkt.Fred Msemwa amesema kwa mwaka 2023/ 24 imeendelea  na ujenzi  wa nyumba  Njedengwa, Magomeni na Gezaulole lengo likiwa ni kupunguza adha wanazozipata watumishi wa umma wakiwemo walimu na manesi 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na timu ya Menejimenti ya   Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) ambapo amewataka  kuja na ubunifu wa kujenga makazi bora ya watumishi wa umma katika maeneo ya mijini  jirani na maeneo ya shule na hospitali  ili kuwaondolea changamoto ya makazi manesi na walimu  kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao  

Sehemu ya  Wajumbe wa timu  Menejimenti ya   Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakimsiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati alipofanya ziara ya kutembelea Makao makuu yaTaasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Mkurugezi wa  Taasisi ya  Watumishi Housing, Dkt.Fred Msemwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati alipofanya ziara ya kutembelea Makao makuu yaTaasisi hiyo Jijini Dar es Salaam


 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakati alipofanya ziara ya kutembelea Makao makuu yaTaasisi hiyo Jijini Dar es Salaam