SERIKALI MTANDAO IMEPUNGUZA GHARAMA ZA HUDUMA KWA WANANCHI NA MIANYA YA
RUSHWA SERIKALINI-Dkt. Mwanjelwa
Na.
Aaron Mrikaria-Dodoma
18
Juni, 2020
Utoaji
huduma kupitia Serikali Mtandao katika Taasisi za Umma nchini umekuwa na tija
kwa wananchi kwa kuwapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika
Taasisi za Umma, ikiwa ni pamoja na kupunguza mianya ya rushwa kwa watumishi
wanaowahudumia wananchi katika taasisi
za umma.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa jijini DODOMA wakati akizungumzia maboresho
ya huduma kwa njia ya TEHAMA yaliyofanywa na Serikali katika Taasisi za Umma
kwa lengo la kuwarahisishia wananchi kupata huduma bora na kwa wakati.
Dkt.
Mwanjelwa amesema, hivisasa wananchi wanaohudumiwa na ofisi yake na katika
baadhi ya Taasisi za umma nchini wanapata mrejesho wa masuala yao kupitia simu
za viganjani au barua pepe zao mara baada ya masuala hayo kupokelewa ili
kushughulikiwa, pasipo kuwalazimu kufika katika ofisi yake na taasisi hizo
ambapo wangelazimika kuingia gharama na hata kuombwa rushwa na baadhi ya
watumishi wasio waadilifu.
“Malipo
ya bili za maji, umeme na mengineyo katika taasisi za umma nchini hufanywa
popote kwa njia ya mtandao, hakika Serikali mtandao imesaidia kuokoa pesa na
muda ambao ungetumiwa na wananchi kwa kupanga foleni ili kulipia bili hizo”,
Dkt. Mwanjelwa amefafanua.
Kuhusu
mapambano dhidi ya Rushwa, Dkt, Mwanjelwa amesema, ukusanyaji wa mapato ya
Serikali umeboreshwa kwa malipo kufanywa kielektroniki hivyo kupunguza mianya,
rushwa na upotevu wa fedha za umma.
Kutokana
na umuhimu wa Serikali Mtandao, naziagiza taasisi zote za umma nchini
kutekeleza matakwa ya Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 ili
kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Taasisi za Umma zinapaswa kuzingatia
kikamilifu matakwa yote ya sheria ya Serikali Mtandao pamoja na kanuni zake
katika matumizi yoyote yale ya TEHAMA yanayofanywa na kuongeza kuwa, taasisi
zitakazo kaidi agizo hili zitakuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Kanuni, Sheria,
Taratibu na miongozo iliyopo” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Aidha
Dkt. Mwanjelwa amezitaka Taasisi za Umma kuwa na utaratibu wa kuwasilisha
mapendekezo ya miradi ya TEHAMA kwenye Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa ajili ya
ushauri na maboresho kabla ya kuanza utekelezaji wake.
Sanjali
na hilo, Dkt. Mwanjelwa amezielekeza Taasisi za Umma kuzingatia viwango na
miongozo iliyoidhinishwa wakati wa usanifu, ujenzi, uendeshaji wa mifumo na miundombinu ya TEHAMA
ili kuhakikisha mifumo hiyo inakuwa na ubora unaotakiwa na usalama wa taarifa.
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliipitisha rasmi Sheria ya Serikali
Mtandao Namba 10 ya mwaka 2019 na tangazo lake kutolewa na Serikali kupitia
tangazo namba 75 katika Gazeti la Serikali ili kuifanya Serikali Mtandao kuwa
mamlaka kamili na hatimaye kutekeleza azma ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa
wananchi na wadau wake kwa njia ya TEHAMA.
|
No comments:
Post a Comment